Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bw. Godfrey Nyaisa amesema Tanzania itaendelea kunufaika na miradi mbalimbali ya Shirika la Miliki Ubunifu Duniani (WIPO). 

Ameyasema hayo katika Mkutano Mkuu wa mwaka wa Nchi Wanachama wa WIPO ulioanza tarehe 4 Oktoba na utahitimishwa tarehe 8 Oktoba, 2021 katika Mji wa Geneva, Uswisi

Katika hotuba yake, Bw. Nyaisa amebainisha miradi ya Miliki Bunifu ambayo nchi ya Tanzania imenufaika ikiwemo kujengea uwezo makundi mbalimbali ili kuweza kutumia Miliki Bunifu kwa maendeleo ya nchi .  

"Mpaka sasa BRELA  imeweka mfumo wa kushughulikia maombi ya hataza na alama za biashara (IPAS), mapitio ya sheria za Miliki Bunifu pamoja na vitabu na  ufundishaji wa sehemu ya Shahada ya Uzamili ya Miliki Bunifu inayotolewa na Chuo kikuu cha Dar es Salaam," ameeleza

Ameongeza kwa kusema kuwa, hivi karibuni WIPO na Mahakama ya Tanzania wamesaini Mkataba wa Makubaliano (MoU) kwa nia ya kuimarisha mfumo wa mahakama na huduma za Miliki Bunifu na ulinzi nchini Tanzania. Utekelezaji wa makubaliano hayo utasaidia kushughulikia changamoto za kisheria zinazohusiana na uamuzi wa Miliki Bunifu unaokabili mfumo wa Mahakama nchini Tanzania

Mkutano huo utapitia na kujadili shughuli mbalimbali na kupitisha bajeti ya WIPO. Tanzania imekuwa mwanachama wa WIPO tangu mwaka 1983.

Imeandaliwa na Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano- BRELA

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bw. Godfrey Nyaisa akiwasilisha taarifa ya Nchi juu ya masuala ya Miliki Bunifu katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Nchi Wanachama wa Shirika la Miliki Bunifu Duniani (WIPO) unaofanyika Geneva, Uswisi kuanzia tarehe 4 hadi 8 Oktoba, 2021

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...