Serikali ya Uturuki imefungua milango ya ushirikiano na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kupitia nyanja kadhaa ikiwemo kujenga uwezo wa watalaamu ili waweze kutoa huduma mpya nchini na kufanya utafiti katika maeneo mbalimbali za kuboresha utoaji huduma.

Hayo yameelezwa leo na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Dkt. Mehmet Gulluoglu alipofanya ziara MNH ili kuona fursa zilizopo za ushirikiano.

Amesema, Serikali ya Uturuki iko tayari kuleta waatalamu katika maeneo ambayo MNH ina upungufu ili kuwajengea uwezo hapahapa nchini na wengine wataenda nchini humo kupata mafunzo mbalimbali kulingana na mahitaji ya hospitali.“Natambua mko kwenye hatua za mwisho za kuanza kupandikiza ULOTO, hivyo ili kufanikisha kuanza kwa huduma hii, sisi tuko tayari kupeleka watalaamu wa MNH kwenda Uturuki wakaone huduma hii inavyotolewa na Hospitali kubwa zenye viwango vya kimataifa na kisha warudi nchini kuanza kutoa huduma hii,” amesema Dkt. Gulluoglu.

Amesema maelefu ya wananchi wanapata huduma kila siku MNH kupitia mawanda mapana ya huduma hizo, hivyo hospitali inahitaji kupewa ushirikiano katika nyanja hizo ikiwemo uanzishwaji wa huduma mpya za tiba, uchunguzi pamoja na upasuaji katika magonjwa mbalimbali.

 Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Prof. Lawrence Museru amemshukuru Dkt.  Gulluoglu kwa ziara yake ambayo imefungua milango ya ushirikiano na kuahidi kutumia vyema fursa zote zitakazotolewa na Serikali ya Uturuki ili kunufaisha wananchi na kupunguza mzigo kwa Serikali kupeleka wagonjwa nje kwa huduma ambazo hazijaanzishwa.

Prof. Museru akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Dkt. Gulluoglu pamoja na wakurugenzi wengine wa MNH.
 
Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Dkt. Mehmet Gulluoglu akieleza jinsi wataalamu wabobezi wa Uturuki watakavyoshirikiana na wenzao wa Muhimbili kutoa huduma za ubingwa wa juu nchini.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akizungumza na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Dkt. Mehmet Gulluoglu. Balozi huyo amesema Serikali yake itasaidia kuboresha huduma za afya ikiwamo ya upandikizaji uloto, upasuaji wa magonjwa mbalimbali na kutoa nafasi kwa wataalamu wa MNH kujengewa uwezo na wenzao wa Uturuki. 
 
Baadhi ya wakurugenzi wa Muhimbili wakishiriki katika kikao hicho.

 

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...