WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Prof Kitila Mkumbo , wawekezaji na Viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya watu wa Czech kuwa Tanzania iko tayari kuwapokea kuja kuwekeza Tanzania  kwa manufaa ya nchi zote mbili.

Waziri Mkumbo ameyasema hayo alipokutana  na  Ujumbe huo ulioongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Czech, Miloslav Stasek pamoja na Martn Klepetko Balozi wa Jamhuri ya Czech nchini Kenya, Krel Tyll Naibu Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Czeck leo 07/10/2021 jijini Dar es salaam.

Prof Mkumbo ameueleza ujumbe huo ulioko utayari  kuwekeza na  kufanya biashara Tanzania katika Sekta ya anga, Ujenzi wa Mitaa ya viwanda, Kilimo na mengineyo  kuwa utayari wa nchi unachochewa na dhamira ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha Tanzania inajikita katika uchumi wa viwanda.

Amefafanua kuwa Serikali imefanya jitihada kubwa mbalimbali ikiwemo kufanyia marekebisho baadhi ya sheria ili kuondoa vikwazo visivyo vya lazima kwa wawekezaji pamoja na ujenzi wa mitaa ya viwanda na jitihadi nyingine nyingi zinazochukuliwa na Mheshimiwa Rais zina lengo la kuhakikisha Tanzania inapiga hatua za haraka katika ujenzi wa uchumi wa viwanda.

Kuhusu uhakika wa soko na usafirishaji wa bidhaa na malighafi Waziri Mkumbo amewatoa wasiwasi kwa kuwaeleza kuwa Bandari ya Dar es Salaam pamoja na uboreshaji wa miundombinu mbalimbali inayofanywa na Serikali inalenga kuhakikisha usafirishaji bidhaa ndani na nje ya nchi kwa haraka na uhakika.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...