Na.Khadija Seif, Michuzi Tv
JUKWAA la Huduma kwa njia ya Mtandao la Mchongoo limepanga kuwaunganisha wafanyabishara na mashirika mbalimbali nchini katika kuwasaidia kuweza kujikwamua kiuchumi.
Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Jukwaa hilo Julius Wambogo amesema wameamua kutumia njia teknolojia ya kidigitali kutokana na kuwa ni njia mpya mpya kwa sasa inayosaidia watu kujipatia huduma mbalimbali.
Wambogo amesema kuwa kupitia Jukwaa hilo la Mchongoo wamekuja na utatuzi wa changamoto mbalimbali kwa wafanyabiashara na makampuni mbalimbali kwa kutoa eneo ambalo wabunifu na watu wanaweza kuonyesha ujuzi wao na hivyo kupata urahisi katika makampuni yao.
‘Tanzania tuna takriban Mill watu 58 na wahitimu wa vyuo kila mwaka ni zaidi ya watu 1000 na tukiangalia uhalisia wahitimu hawa ni wachache wanapata ajira wengi wao huingia mitaani na kuanza kufanya biashara ndogondogo wengine hawana cha kufanya lakini kumbe kuna namna nyingi ambayo wangeweza kuonyesha ujuzi wao,uwezo wao na kipaji chao’amesema Wambogo.
Aidha Wambogo ameeleza kuwa Jukwaa hilo linasaidia pia watu kijipatia huduma mbalimbali sambamba na kuongeza elimu ya watu kuwa na nidhamu kwenye kazi pamoja na bidii.
Amesema kwa sasa Jukwa hilo lipo wazi kwa watumiaji kwani umeundwa kwa ajili ya watu wa aina zote wakiwemo watu wa kwenye Makampuni,,walemavu,watu wa kwenye mataasisi ndani na nje ya nchi na wenye ujuzi na ubunifu kwenye sekta mbalimbali kwani lengo lao ni kuweka urahisi wa kutafuta watu wakati wowote.
‘Ili kusaidia ukuaji na uendeshaji wa Mchongo tunatazamia kushirikiana na mataasisi ya sekta binafsi na mashirika ya wizara za Tanzania na biashara za ndani na njea ya nchi ambayo ina ndoto na mpango wa kuongeza kipato chao na ubunifu wao ili kukuza ukuaji endelevu wa kiuchumi na kumaliza umaskini Afria’ameendelea kusema Wambogo
Hata hivyo amesema wanatarajia kujnga uchumi wa kijamii na wa taifa la Tanzania kwa kutoa njia rahisi za kazi kwenye dimbwi moja la watu wenye ubunifu kwa bajeti ya kuendesha miradi kwa bei nafuu kwa watoa huduma ili kujenga kile kilichoathiriwa na changamoto mbalimbali.
Mkurugenzi wa Jukwaa la huduma kwa njia ya Mtandao la Mchongo Julius Wambogo,jukwaa lenye lengo la kuwaunganisha WAFANYABIASHARA na Mashirika Mbalimbali nchini katika kuwasaidia kuweza kujikwamua kiuchumi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...