Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC). na Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA). Wapo katika maonesho ya kwanza ya Utalii ya Kikanda ya Jumuiya ya Afrika Mashariki nia ikiwa ni kuhamasisha uwekezaji na kueleza fursa za uwekezaji zilizopo nchini Tanzania hususa ni Sekta ya Utalii. Wananchi, wawekezaji na viongozi mbalimbali wametembelea katika banda la TIC na ZIPA na kupatiwa maelezo mbalimbali waliyohitaji, maonesho hayo yanayoendelea jijini Arusha hadi tarehe 16 Octoba, 2021.
Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) wanashiriki maonesho ya Kwanza ya Utalii ya Kikanda ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea jijini Arusha hadi tarehe 16 Oktoba, 2021 kwa lengo la kuhamasisha uwekezaji na kueleza fursa za uwekezaji zilizopo nchini Tanzania.Wananchi, wawekezaji na viongozi mbalimbali wametembelea katika banda la TIC na ZIPA na kupatiwa maelezo mbalimbali waliyohitaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania Dkt. Maduhu I. Kazi amefika katika banda la TIC na ZIPA na kuwahudumia wananchi mbalimbali waliofika katika banda hilo kwenye maonesho ya kwanza ya Utalii ya kikanda ya Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha leo Oktoba 10,2021
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC). Dkt. Maduhu I. Kazi akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) katika banda la TIC na ZIPA kwenye maonesho ya kwanza ya Utalii ya kikanda ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea jijini Arusha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania Dkt. Maduhu I. Kazi alipowasili ktk banda la TIC na ZIPA. Kulia ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA). Bw. Shariff A. Shariff katika maonesho ya kwanza ya Utalii ya kikanda ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoendelea jijini Arusha.
Waziri wa Wizara ya Utalii na Mambo ya kale Zanzibar Mhe. Lela Mohamed Musa ametembelea katika banda la TIC na ZIPA na kuwapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuitangaza Tanzania na Zanzibar kwa Wawekezaji katika maonesho ya kwanza ya Utalii ya Kikanda ya Jumuiya ya Afrika mashariki yanayoendelea jijini Arusha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...