Stanbic yatoa madawati 100 kuboresha elimu

  Benki ya Stanbic Tanzania imetoa madawati 100 yenye thamani ya TZS Milioni 9 kwa Shule ya Msingi Toangoma wilayani Temeke, ikiwa sehemu ya kampeni inayoendelea ya benki hiyo - Stanbic Madawati Inititaive ambayo inakusudia kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuchochea maendeleo ya elimu nchini.

Madawati hayo yalikabidhiwa na Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa Rejareja wa benki hiyo, Omari Mtiga kwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo,  katika hafla iliyofanyika kwenye eneo la shule hiyo jana.

Mtiga alisema benki hiyo  imejikita  kuboresha mazingira ya kujifunzia katika shule tofauti nchini Tanzania, kupitia kampeni ya Stanbic Madawati Initiative, ambayo inakusudia kuchangia madawati 1000 nchini kwa mwaka huu. “Tunaamini kwamba ndoto zote zinawezakana ikiwa zitapewa msaada unaohitajika. Mchango huu utasaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuchochea ufaulu wa wanafunzi wa Toangoma.”

Aliongeza kuwa kampuni hiyo hivi karibuni ilitoa msaada kama huo kwa Shule ya Sekondari ya Mbabala huko Dodoma na ina nia ya kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali kwa kutoa madawati kwa shule katika maeneo mengine ya nchi.

Kwa upande wake, Mhe Jokate alipongeza juhudi za Benki ya Stanbic katika kusaidia serikali kuboresha elimu na akawataka wawekezaji wengine kuiga hatua hiyo.

Alitoa wito kwa uongozi wa shule kuhakikisha kwamba madawati yanatumiwa vizuri, ili waweze kufaidika wanafunzi wengi iwezekanavyo, na pia amewataka wanafunzi kufanya kazi kwa bidii ili kuboresha  ufaulu wa shule.

Mpango wa Stanbic Madawati ulizinduliwa mnamo Julai mwaka huu ili  kushughulikia changamoto ya uhaba wa madawati katika shule kote nchini. Kupitia mpango huo, benki ya Stanbic itatoa madawati 1000 kwa shule za msingi na sekondari katika mikoa tofauti nchini. Kwa kila dawati litakalotolewa, Stanbic itapanda mti ili kutunza mazingira

Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa Rejareja wa benki ya Stanbic Tanzania,Omari Mtiga (Kulia) alikabidhi madawati 100 kwa Mkuu wa wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo (Kushoto) kwajili ya shule ya Msingi Toangoma iliyoko Temeke, hivi karibuni. Hii ni muendelezo wa kampeni ya benki hiyo ya Stanbic Madawati Inititaive ambayo inakusudia kutoa madawati 1000 kwa shule mbalimbali nchini. Hafla hiyo ilifuatiwa na upandaji miti, ambayo ni sehemu ya kampeni hiyo ambayo inakusudia kurejesha mfumo wa ikolojia kwa kupanda mti kwa kila dawati lililotolewa.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...