


Ekwabi Mujungu ambaye ni Meneja Rasilimali Watu na Utawala wa NSSF, akizungumza na wafanyakazi wa Mfuko huo waliokusanyika katika ofisi za Makao Makuu kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja.

Mshereheshaji wa shughuli hiyo, Lulu Mengele ambaye pia ni Meneja wa Uhusiano na Elimu kwa Umma wa NSSF, akitoa utambulisho wa viongozi na waalikwa.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MKURUGENZI Mkuu wa Mfumo wa Hifadhi ya Jamii (NSSF,) Masha Mshomba amesema, azma ya mfuko huo ni kutoa huduma bora na wafanyakazi wa mfuko huo wapo tayari kuwahudumia wanachama na wananchi kwa ufanisi na ubora utakaokidhi matarajio yao.
Mshomba ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja yanayoendelea jijini humo na kueleza kuwa baada ya kuteuliwa wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan Mei mwaka huu ameona kasi na ari ya wafanyakazi wa mfuko huo katika utoaji wa huduma kwa wananchi kwa kuzingatia malengo yaliyowekwa.
"Nimekuwa nikisisitiza juu ya uwazi na uwajibikaji kwa sababu lengo sio kufikia hapa tulipo bali ni kwenda mbele zaidi na kukidhi matarajio ya wateja watu." Amesema.
Aidha amesema kuwa wafanyakazi wa mfuko huo wamekuwa wakifanya kazi kwa ushirikiano na uwajibikaji unaoridhisha na kuwataka kuendelea kufanya kazi kwa kasi hiyo ili kuyafikia malengo.
Vilevile amesema kuwa watahakikisha wafanyakazi wa mfuko huo wanafanya kazi katika mazingira bora kwa kutumia teknolojia na kutoa motisha kwa manufaa ya mfuko na wanufaika wake.
"Kwa kiasi kikubwa tunatumia Tehama tunatarajia wanachama hawatafika katika Ofisi zetu, taarifa zote zitawekwa katika mtandao na kila mwanachama ataweza kufuatilia taarifa zake huko....hii ndiyo NSSF tunaayoitaka na tumeshafikia hilo kwa asilimia 50." Amesema Mshomba.
Pia amesema wamejipanga kutoa elimu kwa wadau ili waweze kuelewa mfuko huo unafanya nini na kutoa huduma zipi ili waweze kujiunga pamoja na kujiuza kwa sekta zisizo rasmi ili kuweza kupata wanachama wengi zaidi.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba, akiongoza matembezi ya amani ya wafanyakazi wa NSSF kutoka Ofisi ya Ilala, Kinondoni, Temeke pamoja na vituo vya Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyobeba kauli mbiu isemayo “NGUVU YA HUDUMA"
Wafanyakazi wakiendelea kusheherekea Wiki ya Huduma kwa Wateja
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba (kushoto), akiwalisha keki baadhi ya wanachama na watu mbalimbali waliofika kupata huduma wakati wa Wiki ya Huduma kwa Wateja.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba, akipokea zawadi kutoka kwa wafanyakazi wakati wa Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyofanyika Makao Makuu ya NSSF Dar es Salaam.Picha ya Pamoja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...