NAIBU Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Kundo A. Mathew alipongeza Shirika la Mawasiliano Tanzania – TTCL Corporation kwa kuendelea kutoa huduma bora za mawasiliano zenye kuleta tija kwa wananchi na Taasisi mbalimbali nchini.
Naibu Waziri ameyasema hayo alipotembelea Banda la TTC
Corporation katika Maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani yaliyoanza leo Oktoba
06 na kutarajiwa kuitimishwa Oktoba 08, 2021 katika Viwanja vya Jakaya Kikwete
Convention Centre jijini Dodoma.
“Serikali tunataka kuona Shirika linaendelea kuongeza juhudi
katika kuwatumikia watanzania kwa kutoa huduma bora zenye ushindani katika soko”
amesema Mhe. Mhandisi Kundo.
Katika Maadhimisho hayo, Meneja TTCL Dodoma, Bw. Samson Marwa
amesema Shirika limeendelea kutekeleza miradi mbalimbali yenye lengo la
kuimarisha huduma za mawasiliano nchini.
“hivi sasa tunaendelea kukamilisha mradi wa kupeleka
mawasiliano vijijini na maeneo ya mipakani ambapo kulikuwa na changamoto za
mawasiliano, hizi juhudi tunazofanya katika kuhakikisha malengo ya serikali ya
kupeleka huduma za mawasiliano zinafanikiwa” amesema Bw. Samson Marwa.
Meneja wa TTCL Dodoma ameongeza kuwa Shirika linatumia Maadhimisho
haya kuwakaribisha watanzania wote kutembelea Banda letu ili waweze kupata
huduma mbalimbali za simu za mkononi, Simu za Mezani, Huduma za Intaneti
kupitia Waya(Fixed broadband) na huduma kwa ajili ya Taasisi na Mashirika.
“Shirika kwa kipindi hiki cha Maadhimisho ya Siku ya Posta
Duniani tunahamasisha matumizi ya simu za mezani kwa wakazi wa jiji la Dodoma
kwa wale wa majumbani na maofisini, huduma hii ni salama na ya uhakika
inayopatikana kwa bei nafuu sana” amesema Bw. Samson Marwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...