Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hasani amesema ziara ya Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye nchini ni muendelezo wa kuimarisha mahusiano mazuri kati ya nchi hizo mbili ikiwemo usalama na kulaani vitendo vya ugaidi.
Rais Samia ameyasema hayo leo Ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma mara baada yakukutana na kufanya mazungumzo na Rais Ndayishimiye ambapo kwa pamoja wamekubaliana ujenzi wa reli na bandari ambazo zinakwenda kuimarisha uchumi wa nchi hizo mbili hasa Burundi kwakua kwa kipindi kirefu ilikua kwenye vita hali iliyochelewesha ukuaji wa uchumi kwa nchi hiyo
Rais Samia amesema Burundi wamenufaika na mkongo wa mawasiliano kutoka Tanzania uliopo mpakani mwa nchi hizo mbili wakati Tanzania itanufaika na ujenzi wa kiwanda cha mbolea ambacho kitaondoa uhaba wa mbolea unaojitokeza kwa wakulima.
Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye akizungumza kwenye mkutano na Waandishi wa Habari Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 22 Oktoba 2021. PICHA NA IKULU.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...