Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) limetoa msaada wa magari mawili (Prado TXL) yenye thamani ya Dola za kimarekani 90,000 ikiwa ni sehemu ya ushiriki wao katika kupambana biashara haramu ya wanyamapori Tanzania.
Mradi huo unatekelezwa na Serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na kituo cha mazingira duniani (GEF) na unakusudia kusaidia kutekeleza mkakati wa kitaifa wa kupambana na ujangili na usafirishaji haramu wa wanyamapori kitaifa na kimataifa.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa makabidhiano Katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Allan Kijazi amesema kwa niaba ya Serikali analishukuru Shirika la UNDP kwa kuweza kutoa msaada huo wa magari yatakayotumika kuweza kusaidia katika kupambana na majangili ili kuweza kuwalinda wanyama.
Pia amesema Serikali itaendelea kutoa elimu kwa Jamii zinazokaa karibu na hifadhi ili kuweza kunisaidia Serikali kwenye ulinzi pamoja na kutoa elimu wa wafanyakazi wa hifadhi ili kuendana na wakati hasa kwenye vifaa yakiwemo magari ya kisasa.
Naye Mkuu wa Kitengo Cha Mazingira kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) nchini Tanzania, Gertrude Lyatuu amesema Shirika hilo ni kiungo Bora kati ya Serikali na rikiana na kituo cha mazingira duniani (GEF) ambao wamefanikisha upatikanaji wa magari mawili kwa ajili ya mradi huo.
Amesema katika nchi kuna wanyama ambao niwa kipee wanaopaswa kulindwa na pia kuhakukisha wanaleta faida kwa taifa hivyo inabidi kuweka nikakati iliyobora hasa ya kutoa vifaa kwa ajili ya mradi wa kulinda na kusaidia kutekeleza mkakati wa kitaifa wa kupambana na ujangili na usafirishaji haramu wa wanyamapori.
Mpango huo umelenga kuendeleza ajenda ya maisha na uhifadhi wa wanyamapori katika sekta ya utalii katika miji na jamii endelevu ya Tanzania na hafla hiyo ya makabidhiano yamezinduliwa na Katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Allan Kijazi na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) nchini Tanzania, Christine Musisi.
Katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Allan Kijazi(kulia) akikata utepe kuadhiria uzinduzi wa magari mawili (Prado TXL) yaliyotolea na UNDP ikiwa ni sehemu ya ushiriki wao katika kupambana biashara haramu ya wanyamapori Tanzania kwa kushirikiana na kituo cha mazingira duniani (GEF). Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) nchini Tanzania, Christine Musisi.
Katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Allan Kijazi akiwasha moja ya gari akishiria uzinduzi wa magari mawili yaliyotolea na UNDP ikiwa ni sehemu ya ushiriki wao katika kupambana biashara haramu ya wanyamapori Tanzania kwa kushirikiana na kituo cha mazingira duniani (GEF) leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Allan Kijazi akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua magari mawili kwa ajili ya Mradi wa kupambana biashara haramu ya wanyamapori Tanzania unatekelezwa na Serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na kituo cha mazingira duniani (GEF) kwa niaba ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP)
Mkuu wa Kitengo Cha Mazingira kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) nchini Tanzania, Gertrude Lyatuu akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya shirika hilo kutoa msaada wa magari mawili ikiwa ni sehemu ya ushiriki wao katika kupambana biashara haramu ya wanyamapori Tanzania hafla ya makabidhiano ilifanyika katika Chuo cha Utalii Mkoani Dar es Salaam leo.
Katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Allan Kijazi na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) nchini Tanzania, Christine Musisi wakiwa kwenye picha ya pamoja wadau mbalimbali wa Mazingira pamoja na Utalii wakati wa hafla ya makabidhiano ya magari ikiwa ni sehemu ya ushiriki wao katika kupambana biashara haramu ya wanyamapori Tanzania hafla ya makabidhiano ilifanyika katika Chuo cha Utalii Mkoani Dar es Salaam leo.
Muonekano wa magari mawili (Prado TXL) yenye thamani ya Dola za kimarekani 90,000 yaliyotolewa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) na ikiwa ni sehemu ya ushiriki wao katika kupambana biashara haramu ya wanyamapori Tanzania
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...