Na Mwandishi Wetu-Arusha


MENEJA wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF),mkoa wa Arusha,Josephat Komba,amewataka waajiri mkoani hapa kuwasilisha michango ya wafanyakazi yao kwa wakati.

Komba ametoa rai hiyo leo Oktoba 8,2021 akizungumza na waajiri,wanachama na wafanyakazi wa mfuko huo,katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya wateja.

Alisema kuwa waajiri wakiwa ni sehemu ya wateja wao wakubwa miongoni mwa majukumu yao ni kuhakikisha wanapoajiri wafanyakazi wao ni kuhakikisha wanawaanidhisha kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii na kuwasilisha michango yao kwa wakati.

“Waajiri ni sehemu ya wateja wetu wakubwa na mna majukumu makubwa matatu ikiwmeo kuhakikisha mnaandikisha wanachama mnapowaajiri,mhakikishe mnafanya makato kwa wakati kama sheria inavyotaka na kuyawasilisha kwa wakati kama ilivyoelekezwa na sheria,”alisema

“Aidha tunaomba ushirikiano wetu pale maafisa wetu wanapokuja kwenye ofisi zenu kuwatembelea kwa ajili ya kuona utekelezaji wa sheria,”

Kuhusu maboresho ya huduma alisema Mfuko huo umejipanga kuboresha na kutoa huduma zake kidigitali ili kuwahudumia wananchi kwa haraka kwa kuzingatia uwazi,weledi na uadilifu mkubwa.

“Katika kuboresha huduma zetu tunaendelea kutoa elimu kwa wateja kwa maana ya waajiri na wanachama juu ya umuhimu wa hifadhi ya jamii na huduma mbalimbali ambazo mfuko unatoa kwa wanachama wake na hiyo inasaidia ganachama hata wanapokuja kufunua madai yao wanakuwa na uelewa huduma zinatolewaje,”alisema na kuongeza

“Wataelewa kanuni na taratibu zingine wakijua hiyo inasaidia kupunguza malalamiko kwa wanachama,wakati mwinmgine wanachama wanalalamika kwa sababu tu ya kutojua taratibu,tumetumia wiki hii kutoa elimu kwa wanachama wetu,”

Alisema maadhimisho hayo yaliyokuwa yakiongozwa na kauli mbiu isemayo “Nguvu ya huduma”,ambapo aliwataka wafanyakazi kutimiza majukumu yao kwa kushirikiana kwa pamoja.

Akizungumzia msamaha wa kodi kwa waajiri ambao wamelimbikiza michango ya wafanyakazi wao,alisema msamaha huo ulioganywa kwa makundi matatu utaanza Oktoba hii hadi Januari 31 mwaka 2022.

“Kundi la kwanza ni wale waajiri wenye malimbikizo ambayo yanaishia Juni mwaka huu,wakiweza kulipa hayo malimbikizo yao yote hadi Novemba 30,waajiri hao watapata msamaha wa tozo kwa asilimia 100,”alisema

“Kwa waajiri ambao watakamilisha malimbikizo ya wafanyakazi wao hadi kufika Desemba 30 mwaka huu,mfuko umeweka utaratibu wa kuwasamehe tozo kwa asilimia 75,na wale waajiri ambao watalipa malimbikizo yao ya nyuma Januari 31,2022 watasamehewa tozo kwa asilimia 50,”

“Tumefanya hivyo kwa kutambua kwamba hapo katikati kulikuwa na kuyumba kwa uchumi kutokana na ugonjwa Corona,waajiri wengi waliathirika kibiashara wengine walishindwa kulipa michango kwa wakati,kwa kutambua hilo mfuko umeamua kutoa msamaha wa waajiri ambao wenye malimbikizo ya michango inayoishia Juni 2021,”

“Ili kuhakikisha tunahudumia wateja wetu mfuko umeendelea kuboresha mifumo yetu ya kitehama,ili kuhakikisha wateja wetu tunawahudumia popote walipo,waajiri wapate huduma wakiwa maofisi kwao na wanachama wahudumiwe wakiwa maeneo yao ya kazi,”

Kwa upande wake mmoja wa waajiri hao kutoka Kampuni ya Elerai Construction,Aziza Mkwata,alipongeza mfuko huo kwa kuboresha huduma zake na kuwa matumizi ya Tehama yamesaidia kuharakisha kupatikana kwa huduma katika mfuko huo.

“Tunawapongeza sana kwa kuboresha huduma zake na kuhamia kidijitali kwnai zimeharakisha utolewaji wa huduma,”alisema

Naye mwanachama Christine Moshi,alisema mfuko huo umekuwa ukitoa huduma zake kwa haraka na ufanisi na kuwa maboresho yake yanasaidia huduma kuwa bora na kuwa wanaupongeza mfuko huo kwa kupunguza tozo hizo waajiri.

Meneja wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF),mkoa wa Arusha,Josephat Komba,aakizungumza na waajiri,wanachama na wafanyakazi wa mfuko huo,,katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya wateja(Picha na Mpiga Picha Wetu)



Afisa Michango wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF),mkoa wa Arusha,Festo Mwakahesya,akiwasilisha mada kuhusu mfumo mpya wa kidijitali kwa waajiri uanowawezesha kupata taarifa,leo katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya wateja(Picha na Mpiga Picha wetu)



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...