NA TIGANYA VINCENT

MKUU wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani amesema zaidi ya wakazi elfu 15 wamejitokeza kuchanja chanjo ya UVIKO 19 katika zoezi linaloendelea kwenye maeneo mbali ikiwa sawa asilimia 50.

Amewataka wakazi wote ambao umri unanzia miaka 18 na kuendelea kuchuka hatua ya kwenda kupata kinga kwa kwa kupata chanjo ya UVIKO 19 ambayo Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Sukuhu Hassan ameileta nchini ili itolewe bure.

Balozi Dkt.Batilda ametoa kauli hiyo leo wakati akitoa elimu kwa wakazi wa Kijiji cha Mtakuja Wilayani Kaliua kuhusu umuhimu wa chanjo ya kujikinga na UVIKO 19.

Alisema chanjo hiyo imedhibitishwa na Shirika la Afya Duniani(WHO) , Wizara ya Afya , Mkemia Mkuu na Mamlaka nyingine zinahusika na masuala yatiba kuwa iko salam.

Balozi Dkt.Batilda alisema katika kudhibitisha hilo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hassan amewaongoza viongozi mbalimbali wa Kitaifa hadi Wilaya kupata chanjo.

Mkuu wa Wilaya Kaliua Paul Chacha alisema katika kuongeza kasi ya uchanjaji kwa kuongeza Vituo kutoka 8 hadi 42 na huduma za mikoba kuwa 20.

Alisema lengo lao ni kuhakikisha huduma zinasogezwa karibu na wananchi ili wasipate shida ya kuzifuata umbali mrefu.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt.Batilda Buriani akitoa elimu leo kwa wakazi wa Kijiji cha Mtakuja wilayani Kaliua ya umuhimu wa chanjo dhidi ya UVIKO 19.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt.Batilda Buriani (kushoto) akisalimiana leo na Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Paul Chacha (kulia) na viongoizi wengine alipowasili kwa ajili ya utoaji wa elimu juu ya umuhimu wa chanjo dhidi ya UVIKO 19.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...