Na Mwandishi Maalum, Kigoma
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria,Profesa Sifuni Mchome amesisitiza kwamba, ni kosa
la jinai kwa mtu yeyote kumsingizia
mtu mwingine tuhuma za ubakaji au unyanyasaji wa kijinsia kwa madhumuni ya kujipatia fedha.
Ametoa maelekezo hayo siku ya
jumatano wakati wa Kikao Kazi na
Kamati zinazoshughulikia
mapambano ya kupinga vitendo vya
ukatili wa jinsia (MTAKUWWA), baada ya
kuelezwa kwamba, kuna baadhi ya wazazi katika Mkoa wa Kigoma ambao wamekuwa
wakitengeneza kesi za ubakaji kama
vitega uchumi.
“Niwaombe sana, mzazi
au mlezi ambaye atabainika kuwa ametumia njia za uongo kutengeneza tuhuma za ubakaji na kisha kujipatia fedha,
huyo anafanya jinai na anapashwa
kuchukuliwa sheria kama mhalifu yeyote yule muanze kufanya hivyo.” akasisitiza
Katibu Mkuu.
Maelekezo ya Katibu
Mkuu Mchome, yalitokana na taarifa za kuwapo kwa baadhi ya wazazi ambao wamekuwa
wakitengeneza matukio ya ubakaji na
kasha kuamua kuyamaliza kifamili na kujipatia fedha.
WP Sakina Rashid
Ndauka ambaye anasimamia Dawati la
Jinsia la Polisi Kigoma Ujiji, alieleza
Kikao Kazi hicho kwamba, sababu za mashauri mengi ya ubakaji kutokamilika ni kutokana na wazazi wawalalamikaji kuamua kumaliza
kifamilia.
Akasema katika mashauri 56 yakiwamo ya ubakaji, ulawiti na mimba za utotoni, ni
mashauri 12 tu yaliyoweza kukamilika
huku watuhumiwa wawili
wakihukumuwa kifungo cha miaka 30 jela.
Hata hivyo Afisa Dawati huyo akasema kuna baadhi ya wazazi ambao wamegeuza matukio ya ubakaji kama kitega uchumi na kujipatia fedha.
Akatoa mfano kwamba
kuna kesi moja ya tuhuma za ubakaji aliyokuwa anaifuatilia, lakini katika mahojiano na Bint aliyetuhumiwa kubakwa, bint yule aliomba azungumze na afisa dawati bila ya wazazi wake
kuwapo.
“ Binti yule aliomba azungumze nami bila ya wazazi wake, na
ndiyo alipokiri kwamba yeye hajabakwa isipokuwa wazazi wake wameitengeneza kesi
hiyo kwa kumfundisha kwamba achukue boda boda kwenda mahali Fulani na kisha wao hutengeneza
mazingira kwamba boda boda yule amembaka na kumfikisha polisi” akaeleza
WP Sakina Ndauka.
Akaongeza kwamba shauri
alipotaka shauri lile
kulifanyia uchunguzi zaidi na hatimaye
kulifikisha mahakani, wazazi wa bint yule waliomba wakalimalize wao wenyewe na
huko ndipo wanapokweda kuchukua fedha.
WP Sakina amesema
ameshakutana na mashauri hayo ya kuwambambikia tuhuma za ubakaji kama
mara mbili hivi.
Akaongeza kwamba, licha ya
familia nyingi kuamua kumaliza
kifamilia matukio ya ubakaji na
unyanyasaji wa kijinsia lakini pia kimekuwapo na visa vya walalamikaji kuwakana
watuhumiwa au mashahidi kukataa kutoa ushahidi na hivyo kuleta ugumu wa
ukamilishaji wa mashauri hayo kwa wakati
na hivyo kujikuta na mlundikano wa majalada.
Kufuatia hali hiyo
hasa ya utengenezaji wa kesi za
ubakaji, ndipo Katibu Mkuu Profesa Sifuni Mchome alipotaka wadau wa haki
jinai kuanza kuwachukulia hatua wazazi
watakaobainika kutengeneza kesi hizo.
Katika hatua nyingine,
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani, Christopher Kadio amewasihi wazee
kutimiza wajibu wao kwa kutoa taarifa
kuhusu matukio yasiyo ya kawaida yanayoendelea katika jamii zao.
Amema wazee wa nchi
hii bado wanasauti na wanapaswa kuzipaza sauti hizo dhidi ya
maovu yanayoendelea katika jamii.
Katibu Mkuu Kadio akabainisha kwamba kuongezeka kwa vitendo
vya ukatili wa kijinsia sababu kubwa inayotolewa
ni mmonyoko wa maadili katika jamii kuwa
mkubwa sana .
“ Mmomonyoko wa maadili katika jamii ni mkubwa sana, kumetokea nini? Na nyinyi wazee mpo, lakini
si kwa wazee wetu tu, kila mmoja wetu ajitafakari na kuchukua hatua” akahimiza Katibu Mkuu Mambo ya Ndani.
Pia akasema serikali inaendelea na mchakato wa kuhakikisha kuwa Polisi Jamii inashuka mpaka ngazi ya Kata. Lakini akasema huduma hiyo haitakuwa na faida ikiwa jamii hazitatoa ushirikiano ili kupunguza uhalifu na ukatili katika jamii
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...