Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Ashatu Kijaji (katikati) akizungumza na Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU), Sifundo Moyo ambaye alimtembelea ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma. Kulia ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dkt Zainab Chaula.
Katika kikao hicho, Katibu Mkuu wa Posta Afrika, Dkt Moyo amempatia taarifa ya utekelezaji wa ujenzi wa Jengo la Makao Makuu ya Posta Afrika jijini Arusha litakalokuwa la ghorofa 17, kuwa hadi sasa ujenzi wake umefikia ghorofa 12.
Dkt. Moyo atahudhuria kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani kesho Oktoba 9, ambayo kwa hapa nchini yatafanyika kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete Dodoma na mgeni rasmi atakuwa Makamu wa Rais, Dkt Philip Mpango.
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...