Na Patricia Kimelemeta-Dar

WAZIRI wa Tamisemi,Ummy Mwalimu amesema anafuatilia suala la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam,kutaka kuwaondoa wafanyabishara wa ndani ya soko dogo la Kariakoo lililopo Jijini Dar es Salaam kwa madai kuwa soko hilo linataka kujengwa.

Hatua hiyo imekuja baada ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam,Hassan Abbas kuwapa siku 10 wafanyabishara hao kuondoka kwenye eneo hilo mpaka ifikapo Oktoba 30 mwaka huu, ili ifikapo Novemba Mosi wazungushe mabati kwa ajili ya kuanza ujenzi, jambo ambalo liliwafanya wamuombe Rais Mama Samia Suluhu Hassan kuingilia kati suala hilo kwa madai kuwa, wanapofanya shughuli zao ni sehemu rasmi linalotambulika kisheria na sio wamachinga.

"Nimepata taarifa kuhusiana na suala la kutaka kuondolewa mwa wafanyabjshara wa soko dogo la kariakoo, nitawasiliana na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam ili anipe ufafanuzi juu ya suala hilo," amesema Ummy..

Hata hivyo ,Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam,Amos Makala aliwataka wafanyabishara hao kubaki katika eneo hilo kwa sababu operesheni inayoendelea ya kuwaondoa wamachinga katika maeneo yasiyo rasmi haliwahusu na kama Luna ujenzi au ukarabati utahitajika katika soko hilo watajulishwa.

"Wafanyabishara wa soko dogo la kariakoo sio wamachinga, hawahusiki na operesheni inayoendelea ya kuwaondoa wamachinga kwenye maeneo yasiyo rasmi kwa sababu wao sio wamachinga, waendelee na shughuli zao kama kawaida na kama kutakua na ujenzi au ukarabati unahitajika, tutawasiliana nao na kuwashirikisha," amesema Makala.

Wakizungumza na waandishi wa habari, Wafanyabishara hao walisema kuwa, uamuzi wa kumuomba Rais Samia kuingilia kati ni baada ya kuona kuwa wameingizwa kwenye operesheni ya wamachinga wakati wao sio wamachinga.

"Tuliitwa na Katibu Tawala,Hassan Abbas na kutuambia tuondoke mahali hapa ndani ya siku 10 kwa sababj wanataka kuanza ujenzi wa soko kuanza Novemba mosi, tumeshangaa sana kwa sababu mpaka maamuzi hayo yanafanyika hatujawahi kushirikishwa wala kuambiwa lolote,badala yake tunaambjwa tutafute maeneo mbadala ya kufanya shughuli zetu ikiwamo buza au kigilagila," amesema Hussein Omary Mwenyekiti wa soko hilo.

Ameongeza kuwa, soko hilo ni la kimataifa ambalo wateja wake wanatoka nchi mbalimbali zikiwamo Kenya,Jamhuri ya Demokrasia ya Congo(DRC),Uganda,Burundi, Rwanda, Msumbiji,Comoro,Madagasca,Zambia,Malawi na nchi nyingine, hivyo basi kuwwpeleka buza au kigilagila ni sawa na kuikosesha serikali mapato.

Ameongeza kuwa, mpaka sasa baadhi ya wafanyabishara waliokua wakifanya shughuli zao katika Soko la Kariakoo lililoungua hawajapa maeneo ya kufanya kazi badala yake wamejibanza katika maeneo ya barabara ili kujitafutia riziki, lakini cha ajabu Serikali ya Mkoa inataka kuwaondoa wao huku wakishindwa kuwapatia maeneo ya bishara wafanyabushara hao.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...