*Wahusia umoja Kati ya Waislaam na Wakristo katika ibada iliyofanyika Kanisa la Sabato Magomeni 

Na Chalila Kibuda ,Michuzi TV

Kanisa la Sabato Magomeni limekaribisha baadhi ya Waislaam wa Magomeni kushiriki ibada ya pamoja ikiwa ni katika kujenga umoja baina ya Wakristo na Waislaam kwa Imani ya kuabudu Mungu mmoja.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa ibada Kanisa hilo Kiongozi wa Shule ya Sabato Magomeni Adam Nyando amesema kuwa Kanisa hilo limekuwa na utaratibu wa kushirikisha Waislaam kwa mwaka mara mbili hali ambayo imejenga mshikamano baina ya Wakristo Wasabato na Waislam.

Nyando amesema dini zetu haziko kwa ajili ya kuchukiana bali zipo kwa ajili ya kumtumikia Mungu kutokana na vitabu vyote vinazungumzia juu ya yeye kutajwa na sio vinginevyo vya kufanya kutoshirikiana katika mambo mbalimbali.

Amesema kuwa licha ya kufanya hivyo kushiriki ibada, bali kuna kuwa na chakula ambacho wanakula pamoja kuonesha umoja zaidi ,ambalo  ndio kusudio la Mungu la jamii kuacha kujitenga.

''Suala la Imani ya dini kila mmoja anayo hivyo kushikamana katika sehemu moja kunajenga utukufu zaidi katika kumtumikia Muumba mbingu na Dunia ambaye ndio wa kuabudiwa pasipo kubaguana kutokana na Imani zetu za dini kati ya wakristo na Waislaam'', amesema Nyando 

Amesema katika utaratibu huo hutambua mahitaji ya watu wanaozunguka Kanisa bila kujali Imani zao kwa kutoa vyakula na mahitaji mengine ya kibinadamu.

Mmoja wa Kiongozi wa Dini ya Kiislaam wa Msikiti wa Kisumo Magomeni Mohammad Kungulilo amesema kuwa utaratibu unaofanywa na Kanisa la Sabato Magomeni ni mzuri, kwani unajenga umoja,udugu na mshikamano kati ya wakristo na Waislaam.

Amesema anayeabudiwa ni Mwenyezi Mungu hivyo kutokuwa  wamoja sio sifa kwani ndio makatazo yake kwa vitabu vyote.

Amesema kuwa baadae kupitia BAKWATA  wanaweza kuwa na mikusanyiko kama hiyo kutokana na maono ya Mufti 

Ibada ikiendelea katika Kanisa la Sabato Magomeni na kukaribibisha viongozi wa dino ya Kiislaam.
Mchanganyiko baadhi ya waumini wa Kiislaam na Sabato katika ibada.

Kiongozi wa Shule ya Sabato Magomeni Adam Nyando akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ibada kati ya  wakristo na Waislaam iliyofanyika Leo .

Kiongozi wa Dini Kiislaam sheikh Mohammad Kungulilo akizungumza kuhusiana na mkusanyiko kati ya Waislaam na Wakristo kufanya ibada ya pamoja

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...