JAJI Mfawidhi Kanda ya Bukoba, Mhe. Dkt. Ntemi Kilekamajenga, amesema, Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba inaweza ikawa inaongoza au ya pili kwa kuwa na kesi nyingi za mauaji.
Jaji Mfawidhi ameyaeleza hayo mwisho mwa wiki ( Ijumaa ) mbele ya Makatibu
Wakuu Watatu waliofika Mahakamani
hapo katika ziara yao ya
Kikazi ya kujionea shughuli za utoaji hakijinai
zinavyotekelezwa katika Mahakama Kuu na Mahakama za Chini Mkaoni
Kagera, mafanikio na changamoto
wanazokabiliana nazo.
Kwa mujibu wa Jaji Mfawidhi Kilekamajenga, ongezeko la kesi za mauaji katika Mkoa huo
ni suala linalofikirisha si kwa Mahakama peke yake bali pia kwa wadau wengine wanaohusika na mnyororo wa uotaji
haki Jinai Mkaoni Kagera.
“Waheshimiwa Makatibu
wakuu, kwanza nitoe shukrani zangu kwa ujio wenu, haijawahi kutokea kwa Mahakama yetu kutembelewa na Makatibu
Wakuu Watatu kwa wakati moja. Nieleze kwamba moja ya changamoto kubwa tuliyonayo ni idadi kubwa ya
kesi za mauaji” Akasema Jaji Mfawishi na
kuongeza
Anaongeza kwamba, wao kama
Majaji na Mahakama kwa ujumla
wamekuwa wakijiuliza sababu za ongezeko la visa hivyo katika Mkoa wa Kagera,
Mkoa ambao unapakana na nchi Jirani tatu, Uganda, Rwanda na
Burund
“Kanda ya Bukoba inaweza kuwa ya kwanza au ya pili kwa
kuwa na kesi nyingi za mauaji,
inafikirisha sana kwa nini kuwa na
visa vingi vya mauaji”. Anaeleza
Jaji Mfawidhi Kilekamajenga.
Akasema Mahakama
Kuu Kanda ya Bukoba hadi sasa ina kesi 249 ambazo zipo tayari kuanza kusikilizwa na
kwamba, na kwamba kesi
49 kati ya hizo zitaanza
kusikilizwa katika kikao maalum cha Mahakama Kuu kitakachoanza Mwezi Novemba
Mwaka hu.
Akabainisha kwamba, uendeshaji wa kesi za mauaji pamoja na
kwamba zipo complicated lakini zinahitaji fedha nyingi kuziendesha kulingana na idadi
ya mashahidi.
Akasema , usikilizaji
wa kesi kumi (10), kwa mfano unaweza kugharimu kati ya shilingi
za Kitanzania milioni 20 mpaka 25
kulingana na idadi ya mashahidi hali inayopelekea kusikilizwa kwa kesi chache
kutokana na ufunyu wa bajeti na
hivyo kuathiri mnyororo wa uotaji haki.
na Akabainisha mbele ya Makatibu hao kwamba, usikilizaji wa kesi kumi (10) kwa mfano , zinaweza kugharimu karibu
shilingi za kitanzania milioni 20 hadi 25 kutegemeana na idadi ya mashahidi.
“ Kesi za mauaji ni
ngumu sana na zinahitaji fedha nyingi sana. Tuna kesi 249 za mauaji, lakini zitakazoweza kusikilizwa ni 49 tu kutonana na
ufinyu wa bajeti, tunaiomba
serikali ione namna ya
kusaidia ili haki iweze
kutendeka na kwa wakati na kupunguza msongamano usio wa lazima katika magereza
yetu”. Akasisitiza Jaji Mfawidhi Imani Kilekamajenga.
Suala la kuwapo kwa
matukio ya mauaji Mkoani Kagera
halikuelezwa tu na Jaji Mfawidhi wa
Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba bali pia
limezungumwa na Mkuu wa Jeshi la
Polisi Mkoa wa Bukoba Kamishna
Msaidizi Awadhi Juma Hajji.
Akizungumzia hali hiyo,
RPC Awadhi Juma Hajji amesema kwa muda mfupi aliokaa Mkoani
Kagera, akiwa ametokeza Zanzibar
amekuwa akipokea taarifa za mauaji na kubwa linalosababisha matukio ya kuuana mkoani
hapa ni wivu wa mapenzi.
Na kwa sababu hiyo
ameshauri kuendelea kutolewa kwa
elimu kwa jamii kuacha kujichukulia
sheria mkononi lakini pia
kila mwananchi katika nafasi yake anapashwa kutimiza wajibu wake ili
kupunguza na kuondoa kabisa matukuo
ya mauaji katika jamii.
“ Muda mfupi ambao
nimekaa hapa nimekuwa nikipata taarifa za mauaji hali si nzuri
sana, wajibu wetu Polisi ni kuhakikisha usalama wa wananchi na mali zao,
ninaomba sana ushirikiano kutoka kwa
wananchi na wadau wengine ya
Hakijinai, na kila mmoja wetu akitimiza wajibu wetu, changamoto
zinazoikabili jamii
zitapungu.Amesisitiza RPC Hajji.
Naye Mwendesha
Mashtaka Mkoa wa Kagera Juma Masanja akizungumzia hali hiyo ya mauaji Mkoani Kagera, licha
ya kusema visa vingine vinatisha
na kushangaza kwamba mwanadamu anaweza kumfanyia hivyo mwanadamu mwenzi
amewataka Maafisa Ustawi wa Jamii na Maendeleo kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya
madhara ya kujichukulia sheria mkononi.
“katika hili na
mimi naomba nichangie, kwa kweli hali si
nzuri, kesi ni nyingi, na wakati mwingine matukio mengine yanatisha na kuogofya
mpaka unashangaa hivi ni mtu anaweza kufanya hivi. Niwaombe Maafisa Ustawi wa Jamii na Maendeleo mtoe elimu kwa
wananchi na muwaeleze kwamba kujichukulia
sheria Mkononi ni Kosa la Jinai” akasitiza Mwendesha Mashtaka Juma
Masanja.
Mmomonyoka wa maadili, watu kutokuwa na hofu ya mungu, wivu wa mapenzi, ulevi wa kupindukia, na migogoro ya ardhi ambayo nayo imeelezwa kuwa ni mingi Mkoani Kagera ni baadhi ya sababu zinazoelezwa kuongeza visa ya mauaji katika mkoa huo.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu
Wizara ya Katiba na Sheria,
Profesa Sifuni Mchome, akizungumza visa
hivyo, amesema takwimu za matukio hayo zinatisha na haziendani na
Nchi ambao imeingia katika Uchumi wa Kati.
“Nchi yetu imeingia
katika uchumi wa kati, lakini bado tunafanya mambo ambayo hayaendani na nchi iliyoingia katika uchumi wakati, tunapashwa
kama jamii kubadilika na ni wazi kuna jambo linatakiwa kufanyika kwa nini jamii
imeingia katika hali hii ya kuuanza” akasisitiza
Profesa Mchome.
Makatibu Wakuu Sifuni Mchome ( Katiba na Sheria), John Jingu ( Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na watoto) na Christopher Kadio ( Mambo ya Ndani) wamehitimisha ziara yao ya kikazi ya wiki moja katika mikoa ya Tabora, Kigoma na Kagera.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...