Kamishna Msaidizi wa Idara ya Ubia kati ya Sekta Binafsi na Umma (PPP), Bw. Bashiru Taratibu, akielezea miradi ya PPP ikiwa ni fursa ya uwekezaji inayotolewa na Serikali kwa Sekta Binafsi kwa Mkazi wa Dar es Salaam, Bw. Clementi Kaaya, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango, katika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayoendelea Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.

Mtaalam wa masuala ya Huduma Ndogo za Fedha kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Joseph Msumule, akitoa elimu kwa Mkazi wa Dar es Salaam, Mzee Juma Mohamed kuhusu umuhimu wa Huduma za Fedha katika ustawi wa jamii, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango, katika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayoendelea Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.

Afisa Mwandamizi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bi. Crispina Nkya, akitoa elimu ya fedha kwa mkazi wa Dar es Salaam, aliyetembelea Banda la Benki hiyo, katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.


Msimamizi wa Fedha kutoka Wizara ya Fedha na Mipango. Bi. Mwanaidi Araba (kulia), akitoa elimu ya Ubia kati ya Sekta Binafsi na Umma (PPP), kwa wakazi wa Dar es Salaam, wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayoendelea Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.

Elimu kuhusu Huduma za Fedha ikitolewa kwa wananchi katika Banda la Benki Kuu ya Tanzania, wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayoendelea Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.


Elimu kuhusu Huduma za Fedha ikitolewa kwa wananchi katika Banda la Wizara ya Fedha na Mipango, wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayoendelea Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.


Mtaalamu wa masuala ya Huduma Ndogo ya Fedha kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Renatus Lucas, akitoa elimu ya huduma hiyo kwa wananchi waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
Mtaalamu wa Masuala ya Mifumo ya Fedha wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Maendaenda, akielezea namna mifumo ya kielektroniki ya malipo ya Serikali inavyofanya kazi, wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayoendelea Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.


(Picha na Peter Haule, WFM, Dar es Salaam)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...