Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

KLABU ya Coastal Union ya Tanga imetoa taarifa ya kujibu hoja iliyozuka kwenye udhamini wa timu za Tanzania kuhusu ‘Fair Competition’ huku wakidai ni mjadala unataka kuihujumu timu yao na kudumaza ustawi wa soka la Tanzania kutokana na wao pamoja na Yanga SC, Namungo FC kudhaminiwa na Kampuni ya GSM.

Taarifa hiyo rasmi iliyotolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano ya Klabu hiyo, imeeleza kuwa mjadala huo huenda ukasababisha timu nyingine kukosa udhamini wa Kampuni mbalimbali, wamedai kuwa ‘Fair Competition’ inayolalamikiwa sio tatizo kwenye udhamini wa GSM.

Taarifa hiyo imedai kuwa aliyeibua mjadala huo hakufanya tafiti na hakuwa na nia njema kwao sambamba na Kampuni zinazodhaminiwa na Kamnpuni hiyo ya GSM.

“Tunatoa rai kwa Wadau wa Soka, Wachambuzi wanapaswa kuibua mada au mijadala itakayohamasisha Makampuni kuwekeza zaidi kwenye soka na si kuharibu sifa za Kampuni hizo na nyingine zenye nia ya kujitokeza kuwekeza kwenye soka letu la Tanzania”, imeeleza Taarifa hiyo.

Pia wadau wa Soka wamekumbushwa ugumu uliokuwepo kwenye soka la zamani ambao ulisababisha timu nyingi kushindwa kumudu gharama za usafiri, mishahara, na masuala mengine, kwa sababu hiyo wanapaswa kuhamasisha Kampuni nyingine kuwekeza kwenye soka la Tanzania.

Hata hivyo, Coastal Union wameomba Shirikisho la Soka nchini (TFF) kukemea mijadala kama hiyo inayolenga kuwaondoa na kukatisha tamaa Wawekezaji katika soka la Tanzania. Pia wamewasihi wawekezaji kupuuza mijadala hiyo isiyo na mashiko na wachukulie kama changamoto.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...