“Wanawake wanayo nafasi kubwa
,Ukimpa mwanamke nafasi ya uongozi ,huwa wanaongoza kwa msingi wa
sheria,hivyo wakiwepo wanawake wengi viongozi nchi za Afrika lazima
zitaendelea"
Na.Vero Ignatus,Arusha
Wanawake
wameaswa kujitokeza na kuwa msatari wa mbele katika kuchukua nafasi
mbalimbali ili kuonyesha uwezo wao na utendaji katika uongozi, kwani
wanawake wakipewa nafasi huwa wanafanya kazi kwa uaminifu
Naibu
Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
anayeshughulikia masuala ya Mipango, Miundombinu, Fedha na Utawala
Mhandisi Steven Mlote ameyasema hayo wakati akifungua kongamano la
mtandao wa wanawake barani afrika la maendeleo na mawasiliano (Femnet)
linalofanyika jijini Arusha.
Mhandisi Mlote aliwataka wanawake popote
pale walipo wajione wao ni viongozi kuanzia ngazi ya familia,mikoa,
Taifa pamoja na uongozi wa jumuiya,ambapo alisema Nyumba ambayo haina
mwanamke hata maendeleo yanalegalega.
“Wanawake popote pale
walipo wajione kama wao ni viongozi na uongozi wao isiishie kwenye
familia zao bali wajitokeze kuonyesha uwezo wao katika kuongoza na sisi
wanaume tuwape nafasi maana mwanamke ukimpa uongozi hana
longolongo”alisema Mlote.
Mhandisi Mlote,alisema kuwa idadi ya
wanawake duniani ni kubwa, hivyo haoni sababu ya wanawake kubaki nyuma
katika suala la uongozi,ambapo aliwakaribisha katika jumuiya ya Afrika
mashariki kuchangamikia fursa za uongozi na kuleta usawa kwa wanaume.
Nae
Mratibu wa WWP Sifisosami Dube kutoka nchini Afrika ya kusini alisema
kuwa, Wanawake wanaoingia katika siasa wanatakiwa kujengewa uwezo pamoja
na ili waweze kufikia malengo ya kile wanachokiendea kwaajili ya jamii
inayomzunguka pamoja na kuwajengea uwezo katika kufanya maamuzi,wanawake
wapo tayari ila kutokana na vikwazo wanavyokutana navyo hawawezi kupiga
hatua
Mwanamke yupo tayari muda wote changamoto inajitokeza pale amabapo anakosa pesa za kufanya kampeni ihawawezi kuwa na nguvu
Vilevile
Spika wa Bunge la Africa Mahariki Martin Ngoga alilitaka Baraza la
Mawaziri, kupendekeza kwa Wakuu wa Nchi wanachama wa Africa Mashariki,
kutoa nafasi ya upekee na kua na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki atakae shughulikia Kipekee Masuala ya Jinsia
Naye
mbunge wa Afrika Mashariki kutoka Nchini Rwanda Fatuma Ndangiza,alisema
usawa wa kijinsia sio suala la wanawake pekee bali ni suala la jamii Kwa
kuwa changamoto kubwa ni tamaduni zetu hivyo jitihada zaidi
zinahitajika katika mshikamano ili kuondoa dhana ya mfumo dume
Mhandisi
Pamela Maasai ambaye ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA)
msemaji wa Umoja wa wanawake katika Bunge la (EALA,)aliwataka wanawake
kutumia fursa za uongozi kuonyesha uwezo wao ili kujenga mazingira ya
kuaminika kwani wanawake wengi Barani Afrika wamekuwa wakisita kugombea
nafasi za uongozi,kutokana na athari za mfumo dume uliojengeka miongoni
mwa Jamii.
Aidha Alisema baadhi ya wanaume wamekuwa vikwazo
katika kutoa ushirikiano kwa wanawake pindi wanapotaka kugombea nafasi
za uongozi wakiamini kwamba mwanamke ni kiumbe dhaifu hawezi kumwongoza
mwanaume jambo ambalo limepitwa na wakati,badala yake wao ndio
wanatakiwa kuwa mfano wa kuigwa kwa kuwatia moyo wanawake pale
wanapoonyesha nia kuwania nafasi hizo.
Kwa upande wake mshiriki
wa kongamano hilo Rose Mjilo kutoka shirika la Mimutie women kutoka
jamii ya kifugaji wilayani Ngorongoro ,alisema changamoto ya mfumo dume
Kwa Jamii ya kimasai bado ni kubwa hivyo elimu zaidi inahitajika ili
kuikwamua jamii hiyo kuachama na dhana hiyo.
AIDHA jamii hiyo
bado inaendekeza mfumo dume wa Uongozi Kwa wanawake na kutolea mfano
kuwa hivi karibuni alijitosa kugombea mchakato wa kupitishwa kuwa
mgombea ubunge katika jimbo la ngorongoro akiwa mwanamke pekee lakini
wanaume walimbeza na kujikuta akikosa hata kura Moja.Naibu
Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
anayeshughulikia masuala ya Mipango, Miundombinu, Fedha na Utawala
Mhandisi Steven Mlote,akifungua Kongamano la mtandao wa wanawake barani
afrika la maendeleo na mawasiliano (Femnet) linalofanyika jijini Arusha.
Spika
wa Bunge la Africa Mahariki Martin Ngoga:Wakuu wa Nchi wanachama wa
Africa Mashariki, kutoa nafasi ya upekee na kua na Naibu Katibu Mkuu wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki atakae shughulikia Kipekee Masuala ya Jinsia
Dkt.Rose
Reuben Mkurugenzi wa TAMWA akizungumza Kongamano la mtandao wa wanawake
Barani afrika la Maendeleo na Mawasiliano (Femnet) linalofanyika jijini
Arusha.Mbunge
wa Afrika Mashariki kutoka Nchini Rwanda Fatuma Ndangiza: Usawa wa
kijinsia sio suala la wanawake pekee bali ni suala la jamii,kila mmoja
anao wajibu wa kuhakikisha napambana kwa pamoja .
Mratibu
wa WWP Sifisosami Dube International Idea kutoka nchini Afrika ya
kusini:Mwanamke yupo tayari muda wote changamoto inajitokeza pale
amabapo anakosa pesa za kufanya kampeni ihawawezi kuwa na nguvu
Mhandisi
Pamela Maasai ambaye ni mbunge wa bunge la Afrika Mashariki
(EALA)“Wanawake tuache woga tujiamini na tugombee nafasi mbalimbali za
uongozi hasa katika nyaja za siasa na tulipata tionyeshe uwezo wetu.
Mkurugenzi
wa TAMWA dkt.Rose Reuben akifuatilia jambo kwa makini katika kikao
Kongamano la mtandao wa wanawake barani afrika la maendeleo na
mawasiliano (Femnet) linalofanyika jijini Arusha
Rose Mjilo kutoka shirika la Mimutie women :kutoka jamii ya kifugaji wilayani Ngorongoro ,alisema changamoto ya mfumo dume
Rachel Kagoya (FEMNET)nchini Kenya:
Ushiriki
katika kampeni za wanawake wanaoongoza Afrika,wanawake katika kufanya
maamuzi ya kisiasa,kutengeneza miongozo ya kuongeza wawakilishi wa
wanawake katika siasa, Majukwaa mbalimbali yanawaunganisha wanawake wa
Afrika kwa pamoja ,kwani mabadiliko wanayoyasema yamechukua muda
mrefu,na wanahitaji kuwekeza zaidi ili kuleta mabadiliko chanya Barani
Afrika
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...