MAHAKAMAya Hakimu Mkazi Kisutu kwa zaidi ya mara tano imeshindwa kuanza kusikilizwa kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka katika kesi ya kughushi cheti cha ndoa inayomkabili Khairoon Jandu.

Hatua hiyo imekuja kufuatia wakili wa washtakiwa Abubakar Salim kutofika mahakamani na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuliitisha jalada la kesi hiyo ofisini kwake.

Awali ilidaiwa kuwa upelelezi dhidi ya kesi hiyo ambayo inasikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Joseph Lwambano ulikwisha kamilika na mashahidi kuandaliwa kwa ajili ya kuanza kutoa ushahidi wao lakini imeahirishwa tena mpaka Novemba 29, mwaka huu ili kuangalia kama DPP atakuwa amerejesha jalada la kesi hiyo mahakamani hapo ama la.

Awali kesi hiyo ilipangwa kuanza kusikilizwa kwa mfululizo kuanzia Novemba Mosi /2 na 3/2021 ambapo mashahidi wa upande wa mashtaka walikwisha andaliwa na wakili wa serikali Ashura Mzava miongoni mwa mashahidi hao yumo Wakili wa kujitegemea Jerome Msemwa lakini ilishindikana baada ya DPP kuliitisha jalada la kesi hiyo.

Msemwa ambaye ni shahidi wa upande wa mashtaka alitarajiwa kuanza kutoa ushahidi wake kwenye kesi hiyo ya kughushi cheti cha ndoa inayomkabili Khairoon Jandu Novemba Mosi mwaka huu lakini alikwama kufuatia hatua hiyo ya kuitishwa kwa jalada.

Awali kabla ya jalada la kesi hiyo kuitishwa na DPP kesi hiyo ilikwamba kuanza kusikilizwa kwa sababu wakili mshtakiwa, Abubakar Salim alikuwa na udhuru …Kwa mujibu wa taarifa iliyofikishwa mahakamani hapo wakili huyo alikwenda kuhudhuria kesi Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi.

Kufuatia taarifa hiyo,Wakili wa serikali Ashura Mzava alidai ni mara ya tano sasa kesi inashindwa kuanza kusikilizwa kwa sababu ya wakili wa utetezi kutofika mahakamani.

“Mheshimiwa hakimu pamoja na wakili kuleta taarifa hii lakini naona kuna mchezo anafanya hii ni mara ya tano sasa kesi inashindwa kuendelea kwa yeye kutofika mahakamani naandaa mashahidi lakini wakili haonekani mahakamani” alidai wakili Mzava.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...