* DC Gondwe asema wapo pamoja katika kufanikisha matumizi ya mfumo huo


MKUU Wa Wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe ameahidi ushirikiano kwa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini TARURA,) katiika mfumo wa ukusanyaji wa ushuru wa maegesho ya magari kwa njia ya kielektroniki utakaoanza kesho Desemba mosi katika mikoa ya Dar es Salaam, Iringa, Dodoma,Mwanza, Singida na Dodoma.

Akizungumza katika kikao maalumu cha kuwajengea uwezo kilichowakutanisha Wakala hiyo, Madiwani na kamati ya Ulinzi na Usalama wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Gondwe amesema kuwa ushirikishwaji wa viongozi hao katika masuala ya kijamii ni muhimu kwa kuwa viongozi hao ni kiungo muhimu waliokaribu za wanajamii hasa kwa kuwapa elimu na maelekezo yanayotolewa kutoka Serikali na wadau wa maendeleo.

Gondwe amesema mfumo huo wa ukusanyaji ushuru wa maegesho ya magari ni muhimu na salama kwa mapato ya Serikali ambayo pia yatatumika katika kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo barabara, madarasa na vituo vya afya na kuishauri Wakala hiyo kuweka alama maeneo yote ambayo wanakusanya mapato ili kuweka sawa sitofahamu ya wapi Wakala hiyo inakusanya mapato hayo.

Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Songoro Mnyonge ameipongeza TARURA kwa kutoa elimu hiyo kwa viongozi hao na kuwashauri mapato yatakayokusanywa katika Manispaa ya Kinondoni yarejeshwe kwa kutekeleza miradi mbalimbal;i ya kimaendeleo hasa miundombinu ya barabara.

Awali Mwanasheria wa TARURA Bonaventure Mwambaja amesema kuwa wamejipanga na wataalam wanaendelea kutoa elimu kwa makundi mbalimbali wakiwemo wakusanyaji wa mapato ambao wametakiwa kuwa waamifu na wenye kauli nzuri za wateja.

Amesema malengo ya mfumo huo ni yenye kuifaa jamii na kujenga taswira nzuri kwa Serikali kwa kukusanya maapato kwa uaminifu na kuyaelekeza katika miradi itakatowanufaisha wananchi na kuwataka wananchi kuwasilisha malalamiko katika ofisi za TARURA za Wilaya na Mikoa zinazopatikana kote nchini.




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...