Na Mwandishi Wetu
KAMA sehemu ya mkakati wake, kuongeza shehena ya mzigo toka nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imetembelea mpaka wa Kasumbaresa kujionea shughuli za mpakani hapo.
Mpaka wa Kasumbaresa ambao hupakanisha nchi za Zambia na DRC, ndio mpaka mkubwa unaopitisha shenena kubwa ya bidhaa zinazotoka na kuingia nchini DRC kupitia Bandari ya Dar es Salaam.
Menejimenti ya TPA iliyoongozwa na Mkurugenzi Mkuu Eric Hamissi iliambatana wadau kadhaa katika ziara hiyo iliyolenga kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wateja wanaotumia bandari za Tanzania ili kuongeza ufanisi wa utoaji huduma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...