MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP,) umeandaa Warsha kwa viongozi Wanawake na Vijana wa kike kuhusu umuhimu wa uingizwaji na utekelezaji wa masuala ya kijinsia katika vyama vya siasa 2021.
Warsha hiyo imeandaliwa kwa lengo la kujenga uelewa wa pamoja juu ya umuhimu wa ushiriki wa wanawake katika kutoa maamuzi na uongozi katika miundo ya uongozi. Pia kujadili na kuthamini uchambuzi juu ya masuala ya kijinsia yaliyo ingizwa katika miundo wa vyama vya siasa na kujenga uelewa wa pamoja juu ya Sheria ya vyama vya siasa.
Akiwakilisha mada mratibu wa Taifa mtandao wa Ulingo Dr.nAve
Maria Semakafu amewaasa wanawake kujitathmini kuona fursa zilizo mbele yao wajitokeze zaidi
kuwania nafasi za uongozi.
Bi Ave Maria amewashauri wanawake kujiwekea utamaduni wa kujitatathimini
waonapo changamoto wanazotakiwa kuzifanyia kazi na kuona jinsi gani ya kuzitatua.
Lakini pia amewashauri wanawake viongozi kuwa pamoja kuacha tofauti
za kivyama na kuwa na umoja .
Kwa upande wake Mkurugenz Mtendaj wa TGN B. Lilian liundi ametoa takwimu juu ya hali ya uongozi uwakilishi wa wanawake katika ngazi za maamuzi ya uongozi na kueleza kwa bado hawajafika lengo na kueleza kuwa TGNP imekuwa ikitengeneza mikakati ya pamoja ya namna ya kuongeza kasi ya utekelezaji wa masuala ya kijinsia kwa vyama vya kisiasa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...