Mwandishi wetu, Arusha
MRADI wa kuwajengea uelewa na ujasiri wanawake vijana walioko kwenye taasisi ya elimu ya juu kuweza kumiliki na kutumia mitandao ya kijamii kwa ajili ya kudai haki za kijamii, kisiasa na kiuchumi wanafunzi umezinduliwa jijini Arusha.
Mradi huo unashirikisha mashirika be matatu.Shirika la wanahabari la utetezi wa jamii za pembezoni ( MAIPAC),Taasisi ya Uraia na Msaada wa Kisheria (CILAO) na Shirika la Kusaidia Ustawi wa Wanawake na Watoto (WOCWELS)
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Taasisi ya Cilao Odero Charles amesema vyuo vikuu vinavyohusika Tumaini Makumira Mtakatifu Agostino Centa ya Arusha na Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru-TICD.)
Amesema lengo la mradi huo ni kuwajengea uelewa na ujasiri Wanawake Vijana walioko kwenye Taasisi ya elimu ya juu kuweza kumiliki na kutumia mitandao ya kijamii kwa ajili ya kudai haki za kijamii, kisiasa na kiuchumi.
" Tunawataka wanawake vijana waliopo Elimu ya juu kutumia vyema vitandao Kwa kupaza sauti dhidi ya ukatili wanaofanyiwa vyuoni" Odero Charles.
Mkurugenzi wa Shirika la MAIPAC Mussa Juma amesema katika mradi huo, kutakuwa na kampeni katika vyombo vya habari na Mitandao ya kijamii.
Amesema pia kutakuwa na mafunzo kuhusu usalama na ulinzi kwenye mitandao ya kijamii na kuhakiki usahihi wa taarifa.
"Wasichana mliopo kwenye Taasisi za elimu ya juu, msiwe wanyonge katika kumiliki na kutumia mitandao ya kijamii kwa ajili ya kudai haki za kijamii, kisiasa na kiuchumi," amesema Juma.
Mkurugenzi wa Shirika la WOCWELS Mary Mushi amesema katika mradi huo kutakuwa ja mafunzo kuhusu Sheria na Sera zinazolinda matumizi ya Mitandao nchini.
"Pia kutakuwa na dahalo kuhusu matumizi ya dijitali na fursa hivyo tunataka wasichana kwenye Taasisi za elimu ya juu kutumia mitandao vizuri na tutatumia hashtags.maisha salama,fursa zaidi na digitali,"amesema.
Wakizungumza katika uzinduzi huo, viongozi wa serikali za wanafunzi vyuo Cha St Agostini, Makumira na taasisi ya maendeleo ya jamii Tengeru walieleza watashirikinvyema mradi huo kwani unamanufaa kwao.
Awatif Mshana ambaye ni Waziri wa Afya SAUT Arusha alisema wanachuo wasichana wamekuwa waoga katika kutumia mitandao kutokana na baadhi ya watu kunitumia kuwadhalilisha.
"Tunaamini elimu hii itakwenda kutuunganisha wanachuo wasichana na kutumia vizuri mitandao"amesema.
Ester Koka mwanafunzi chuo kikuu cha Tumaini Makumira alisema wanasichana wengi chuoni wamekuwa hawatumii vizuri mitandao lakini yeye anatumia vizuri na amenufaika kupata fursa mbalimbali.
Mwanafunzi chuo Cha Maendeleo ya jamii Tengeru Joyce Athanas alisema anaimani Kupitia mradi huu atakwenda kutumia mitandao vizuri na kupaza sauti juu ya ukatili vyuoni.
Mwanafunzi wa SAUT Arusha Ruth Usanga aliwasilisha wanachuo wenye ulemavu alisema wengi wao wapo vijijini hawajuwi fursa zilizopo kwenye mitandao hivyo atakuwa balozi mzuri kumfikisha elimu vijijini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...