*STAMICO yaweka mikakati ya kuwainua wachimbaji wadogo wa madini.

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
SHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO)na Benki ya NMB wametiliana saini ya mashirikiano na makubaliano kwa lengo la kuwainua wachimbaji wadogo kupitia sekta ya madini kuwapatia mikopo kwa ajili ya kununua vifaa.

Makubaliano hayo yamefanyika katika ofisi za Makao Makuu ya Shirika la Taifa Madini (STAMICO) ambapo Shirika limesema huo uendelezaji wa mkakati wa Shirika kwenda kumshika mkono mchimbaji mdogo kwenda kuwa mchimbaji mkubwa kutokana fursa zilizopo kwa kushirikiana Taasisi za Kifedha.

Akizungumza katika hafla hiyo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dk. Venance Mwasse amesema hadi kufikia sasa wao kama shirika wameshatoa leseni 34000 kwa wachimbaji wadogo ambao ni wazawa hapa nchini ambao wanakwenda kunufaika mikopo ya vifaa kutoka Benki ya NMB.

Mwasse amesema ili kuchochea ukuaji wa uchumi kwa wachimbaji wadogo kupata faida ni kutoa fursa ya kuwakopesha wachimbaji hao na Benki ya NMB wanapenda kupata wateja ili fedha iweze kuzunguka.

Dkt. Mwasse alifafanua kuwa madini kama hayachimbwi kunakuwa hakuna maana yeyote hivyo amewaomba NMB kutoa fursa ya mikopo kwa wachimbaji hao wadogo.

"Makubaliano haya yanakwenda kuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi kwa wachimbaji na yanakwenda kunufaisha wote wawili kwa maana ya benki na wachimbaji hawa ambao ni wateja"Amesema Mwasse.

Aliongeza kuwa muafaka huo unakwenda kutengeneza ukuaji wa kodi na kubwa zaidi kutakuwa na mzunguko mkubwa wa fedha na shirika linakwenda kunufaisha wachimbaji wadogo huku akiwataka wachimbaji hao kubadilika na kufuata sheria.

Kaimu Mkurugenzi huyo amesema biashara ni ushindani na hivyo kitendo cha kuingia makubaliano na taasisi za fedha ni mpango kababe ambao lengo lake hasa ni kutaka kuwasaidia wachimbaji wadogo na ndio maana siku chache zilizopita walikubaliana na GST kwa maana wao ndio watalaamu ambao wanajua wapi mahala ambapo pana madini.

Amesema wao kama Stamico wamenunua mashine tano kwa ajili ya kuchoronga madini na mashine hizo ndio mwarobaini na wakishachoronga wanakwenda kupima na kupata uhakika wa uwepo wa madini katika eneo husika .

Alisema huo ni mwazo na wataendelea kununua mashine kwa ajili ya wachimbaji wadogo na huko nyuma mchimbaji mdogo ilikuwa kama shida hivyo wameamua kuwashika mkono na wanatarajia kuleta muwekezaji kutoka nje ya nchi ambayo atakuja pia kusaidia wachimbaji hao wadogo.

Kwa upande wake Afisa Mkuu wa Mikopo kutoka NMB Daniel Mboto aliwashukuru Stamico kwa kukubaliana kuwa pamoja katika kuhakikisha wachimbaji wadogo wananufaika na nmb.

Alisema NMB kwao ni mwendelezo kwani hata wao wapo kwenye maeneo mbalimbali ya migodi na ushirikiano huo ndio umefikia leo kuingia kwa mara nyingine na stamico kwa ajili ya wachimbaji wadogo.

Amesema taasisi za fedha zipo kwa ajili yo na amewataka kujitokeza kwa mameneja wa mikopo ili kupata taarifa zao ambazo zitawawezesha kupata fedha au mikopo kupitia NMB.

Ameongeza kuwa kwaupande wa shirika la madini ni kuwa na taarifa sahihi za mchimbaji huyo ili hata atakapokuja kwao kwa ajili ya mikopo aweze kuaminika na kupata mkopo kwa ajili ya shughuli zao za uchimbaji .

"Nawashukuru sana STAMICO kwa kufikia makubaliana haya ambayo yanakwenda kuwa na tija katika nchi na kwa wachimbaji hawa wadogo." amesema

Amesema wao kama NMB wanamikakati ya muda mrefu na mfupi na waliweka milioni 123 na hivi sasa wameshatoa mikopo hadi milioni 20 na kwa makubaliano hayo wataendelea kasi ya kukopesha.

Kuhusu mikopo amesema mkopo kwa kutumia wadau wao ambao ni STAMICO, Benki itatoa mikopo rafiki kwa wachimbaji na wadau mbalimbali wa sekta ya madini.

Mbotto amesema pia watatoa elimu ya fedha kwa wadau katika sekta ya madini ili kusaidia katika kuhakikisha matumizi sahihi ya fesha yanafanyika.

"Ni fursa ya kipekee sana kwa wachimbaji wadogo na wadau wa sekta ya madini kwani kwa kila hatua ya shughuli zao, benki ya Nmb na Stamico tuko nao kuhakikisha wanafanikiwa." alisema

Alifafanua kiwa mteja anapata muongozo wa namna ya kuwekeza na wapi pakuwekeza kutoka STAMICO, baadae benki ya NMB inampa mkopo rafiki kabisa wakati mteja anaendelea na shughuli zake.

"Nitoe rai kwa wadau wa sekta ya madini kuchangamkia fursa hii na watembelee matawi ya Nmb kwa ajili ya maelekezo ya mikopo ambayo kwa sasa itakuwa na baraka na miongozo kutoka STAMICO na kuwafanya wapige hatua mbele zaidi katika biashara na shughuli zao." alisema

Kwa upande wake mwakilishi wa wachimbaji wadogo Salma kundi kutoka TAWOMA aliwashukuru STAMICO na kwamba kwao ni siku ya kihistoria na kwaniaba ya wachimbaji wadogo wote amesema wao watajitahidi kwakufuata utaratibu wote ili waweze kunufaika.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Stamico Dk.Venance Mwasse na Afisa Mkuu wa Mikopo wa Benki ya NMB  Daniel Mbotto  wakionesha hati ya makubaliano  mara mara baada ya kusaini.
Picha ya pamoja kati ya Watendaji wa Stamico na Benki ya NMB mara baada ya kusaini makubaliano ya kuwakopesha wachimbaji wadogo wa madini yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Stamico Dk.Venance Mwasse na Afisa Mkuu wa Mikopo wa Benki ya NMB Daniel Mbotto wakisaini makubaliano ya kuwakopesha wachimbaji wadogo wa madini katika hafla iliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
Afisa Mkuu wa Mikopo wa Benki ya NMB Daniel Mbotto akizungumza juu ya Benki hiyo kutoa mikopo ya wachimbaji wadogo wa madini mara baada ya kusaini makubaliano na Stamico katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Taifa la Madini (STAMICO) Dk.Venance Mwasse akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuingia Makubaliano na Benki ya NMB kwa ajili ya kuwakopesha Wachimbaji Wadogo wa Madini katika hafla iliyofanyika Ofisi za Stamico jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Stamico Dk.Venance Mwasse wakibadilishana hati ya Makubaliano na Afisa Mkuu wa Mikopo wa Benki ya NMB Daniel Mbotto  katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...