Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi, Mhandisi Consolata Ngimbwa akitembezwa kwenye maeneo mbalimbali ya mradi wa umeme wa Megawati 2115 wa Julius Nyerere (JNHPP), ulioko Rufiji Mkoa wa Pwani wakati ujumbe huo ulipotembelea mradi huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB), Mhandisi Consolatha Ngimbwa na Msajili wa Bodi hiyo, Mhandisi Rhoben Nkori wakimsikiliza mmoja wa wafanyakazi wa Tanesco wanaosimamia mradi wa kuzalisha umeme wa Megawati 2,115  wakati yeye na ujumbe wake walipotembelea mradi huo Rufiji Mkoa wa Pwani.
Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB), Mhandisi Consolatha Ngimbwa wa pili kutoka kushoto akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wengine wa bodi hiyo na wale wa Shirika la Umeme Tanesco kwenye mradi wa kuzalisha umeme wa Megawati 2115.
Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB), Mhandisi Consolatha Ngimbwa katikati akizungumza na viongozi wa Tanesco wanaosimamia mradi wa kuzalisha umeme wa Megawati 2,115 wakati yeye na ujumbe wake walipotembelea mradi huo Rufiji Mkoa wa Pwani.


Na Mwandishi Wetu, Rufiji
WAJUMBE wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB), wametembelea mradi wa mkubwa wa bwawa la kufua umeme wa maji la Julius Nyerere (JNHPP) uliiopo Rufiji mkoani Pwani.

Lengo la ziara hiyo ilikuwa kujua maendeleo ya mradi na kujionea hatua mbali mbali za utendaji kazi unaofanywa na kampuni ya Arab Contractors kwa pamoja na Elsewedy Electric zote kutoka nchini Misri.

Kampuni hizo mbili za kigeni zinatekeleza mradi huo chini ya usimamizi wa Wizara ya Nishati, Shirika la Umeme (TANESCO) na Wakala wa Barabara Nchcini (TANROADS).

Wajumbe hao wa Bodi wakiongozwa na Mwenyekiti Mhandisi Consolata Ngimbwa wameonyesha kufurhishwa kwao na maendeleo ya ya mradi huo na kujifunza mambo mengi.

Pia Mwenyekiti wa Bodi ya CRB, Mhandisi Consolata Ngimbwa amezitaka kampuni hizo za kigeni kuhakikisha zinatoa nafasi za ushiriki wa miradi mbalimbali inayoitekelezwa ili kuziinua kampuni za kizalendo zilizopo nchini.

“Mradi huu ni mkubwa sana na una kazi nyingi sana hivyo anaona fursa ipo kwa makandarasi wazawa kuepwa kazi ndogo ndogo kama sub – contractors” alisema.

Pia amezitaka kampuni zinazohusika na masuala ya ukandarasi hapa nchini kujenga ushirikiano wa pamoja ili kuwa na nguvu ambazo licha ya kuzisaidia kupata mitaji mikubwa itawawezesha kufanya kazi kwa kipindi kifupi na ufanisi utakaoleta matokeo chanya katika mradi husika.

Bwawa hilo linatarajiwa kuzalisha Megawati 2,115 na kwa sasa mradi huo umefikia asilimia 48.2 .

Kukamilika kwa mradi huo kutawezesha Watanzania kupata umeme wa gharama nafuu ambao utasambazwa nchini kote na ziada kuuzwa nje ya nchi ili kupata faida za kigeni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...