MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud, ametoa mkono wa pole kwa Mama Awena na familia yake kufuatia kifo cha mzazi wao mapema wiki hii.

Mhe. Othman amewasili Mwera Mtufaani Wilaya ya Magharib 'A', Mkoa Mjini Maagharib Unguja, ilipo familia ya Mama Awena, mara tu baada ya sala ya Ijumaa ili kuwafariji wafiwa.

Mama Awena ni mjane wa Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad, ambaye aliwahi kushika nafasi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kwa awamu mbili tofauti, kuanzia 2010 - 2015, na baadaye Disemba, 2020 - Februari,2021 alipofariki dunia.

Mzazi huyo wa Mama Awena, Mzee Sinani Masoud alifariki nyumbani kwake Mwera mtufaani na kuzikwa kijiji cha Mgeni haji wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Awali Mhe.Othman alijumuika na waumini wa dini ya kiislamu kwaajili ya ibada ya sala ya ijumaa iliyosaliwa katika Mskiti wa 'MUSTAQIM' Kijichi pia katika Wilaya ya Magharib A, Mkoa wa Mjini Magharib Unguja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...