Jane Edward, Arusha.

Rais Samia Suluhu Hassan amezindua rasmi hoteli ya kisasa ya nyota tano Gran Melia Arusha, huku akialika wawekezaji zaidi kwenye sekta ya Utalii nchini.

Rais Samia Suluhu amezindua rasmi hoteli ya kisasa ya nyota tano Gran Melia katika jiji la Arusha, huku akialika wawekezaji zaidi kwenye sekta ya Utalii nchini.

Akizungumza katika uzinduzi huo , Rais Samia amesema Tanzania ni eneo bora na Salama kwa kuwekeza kutokana na kuwa na vivutio vingi vya utalii huku ikitenga asilimia 32.5 ya ardhi katika uhifadhi na utalii.

Amesema Serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri ya kuvutia wawekezaji huku akawaalika taasisi ya Albwardy ambao ndio wamiliki wa hoteli kuwekeza zaidi hapa nchini.

Amesema Tanzania ni salama na hata kipindi hiki cha janga la uviko-19 imekuwa salama kutokana na kuzingatia tahadhari zote za kupambana na uviko-19.

Rais amesema miongoni mwa tahadhari hizo ni kuchanja ambapo yeye binafsi alizindua zoezi hilo mwezi Julai kwa kupata chanjo.

“Tanzani ni salama tunawakaribisha kuwekeza na kutembelea na mtaondoka salama”amesema Rais Samia

Amesema kutokana na Tanzania kuzingatia viwango vya kupambana ma uviko-19 imepewa tuzo kadhaa na mashirika ya kimataifa ya utalii na kutajwa kama kituo salama cha kutalii.

Amesema pia hifadhi za Taifa ikiwapo Serengeti imeendelea kupata tuzo kama hifadhi bora zaidi Afrika 2020 na awali pamoja na hifadhi ya Ngorongoro na mlima Kilimanjaro zilipata tuzo ya hifadhi bora na miongoni mwa maeneo ya maajabu ya asili barani Afrika .

Awali Waziri wa Maliasili na Utalii,Dk Damas Ndumbaro aliwapongeza Gran Melia kwa kuwekeza nchini hotel 6 za kitalii na kufanya Tanzania miongoni mwa nchi 40 ambazo kampuni hiyo imewekeza hoteli 350.

Hata hivyo ameomba kampuni hiyo kuwekeza hoteli nyingine tatu na kufanya ziwe tisa kama ilivyo katika nchi nyingine.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa hoteli hizo, Ally Albwardy alishukuru serikali ya Tanzania kwa kusaidia wao kuweza kuwekeza hapa nchini.

Amesema kwa sasa wafanyakazi 800 wameajiriwa katika hoteli zao huku akiahidi kutoa huduma bora za hadhi ya nyota tano .
Rais Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria ufunguzi wa hotel ya Gran Melia jijini Arusha (Picha na Jane Edward, Arusha)
Rais Samia akihutubia  wadau wa utalii mara baada ya kufanya ufunguzi wa hotel hiyo (Picha na Jane Edward, Arusha)
Rais Samia akiwa Kwenye picha ya pamoja na wadau wa Utalii (Picha na Jane Edward, Arusha)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...