Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
SERIKALI kupitia Wizara ya Utamaduni , Sanaa na Michezo imezindua Bodi ya Mfuko wa utamaduni na sanaa , mifumo ya kidigitali ya Baraza ya BASATA, Bodi ya Filamu,COSOTA pamoja na mashindano ya Samia Taifa CUF.
Akizungumza katika Ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam Waziri wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa amesema wamekutana leo Novemba 22,2021 kwa ajili ya kuzindua bodi ya mfuko wa utamaduni na sanaa, mfumo wa kidigitali wa BASATA , Mfumo wa kidigitali wa Bodi ya Filamu, Mfumo wa kidigitali wa COSOTA,mashindani ya Samia Taifa CUP pamoja na kuongeza na kuimarisha wigo wa Serikali kufanya kazi na wadau wa tasnia hizo.
"Leo ni siku ya kihistoria kwani tunakwenda kuiona ile ndoto ya Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi madhubuti na mahiri wa Mama yetu Rais Samia Suluhu Hassan ikitafsiriwa kwa vitendo,Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo itaendelea kujenga mazingira rafiki na wadau wa shughuli za utamaduni , sanaa na michezo ili wavune matunda ya kazi zao kupitia vipaji vyao,"amesema Waziri Bashungwa.
Amesema ni kweli leo wanapozindua mifumo , bodi na mashindano hayo ya michezo , wanaendelea kukumbusha kuwa hizo zote tatu ni sekta za kimkakati kwa Taifa lolote, sekta hizo zina tasnia zinazozalisha ajira rasmi, na siziso rasmi kwa wananchi wengi na kuwezesha kupata kipato cha kujikimu kimaisha na kwamba hivi sasa kimezaliwa kitu kinachoitwa uchumi bunifu.
"Uchumi huo ni moja ya nguzo za uchumi wa Taifa lolote duniani linalotaka kuwa na uchumi imara na wenye tija kwa watu wake, wakiwemo wa hali ya chini kwasababu ya ukweli huo , serikali inaona upo umuhimu wa kujenga mazingira rafiki zaidi na wezeshi kwa sekta hizi za utamaduni, sanaa na michezo ili kuhakikisha zinazidi kukua na zinabaki imara,"amesema.
Kuhusu bodi ya mfuko wa utamaduni, sanaa na michezo, Waziri Bashungwa amesema kwa kutambua thamani na nafasi ya sekta hizo Serikali imeamua kufufua mfuko uliokuwa ukijulikana kwa jina la Mfuko wa Utamaduni Tanzania ulianzishwa Agosti 28 mwaka 1998 kwa hati ya utamaduni(culture Trust Fund).
Amefafanua mfuko huo baadae ulififia na kufa kwasababu mbalimbali , hivyo kuanzisha mfuko wa Utamaduni, Sanaa na Michezo tena chini ya Serikali ya sasa siyo maagizo tu na dhamira ya Rais bali ni kuitikia kilio cha wadau kuhusu kuwa na mfuko utakaosukuma mawazo yao, miradi yao na ubunufu wao.
Waziri Bashungwa akizungumzia mifumo ya taasisi ,amesema anayo furaha kueleza wanakwenda kuzindua mifumo mipya ya kidigitali kwa ajili ya wasanii nchini, mifumo ambayo wadau wameonesha na imeelezwa na watalaam na itahusu taasisi za baraza la sanaa la Taifa(BASATA)Bodi ya Filamu Tanzania na ile ya COSOTA."Wasanii na wadau wengine wameteseka , kila kitu kwenda mguu kwa mguu kufika ofisini kupata utatuzi , nimpongeze Katibu Mkuu Dk.Hassan Abbas na timu nzima ya wakuu wa taasisi hizi kwa kushirikiana na Wakala wa Serikali mtandao kuratibu na kushirikiana kujenga mifumo hii na pale kwenye changamoto na marekebisho zijulisheni taasisi tuboreshe, naziagiza BASATA, BFT na COSOTA kuendelea kutoa elimu kuhusu mifumo hii."
Kuhusu Samia Taifa CUP , Waziri Bashungwa amesema kama ilivyoelezwa , wamezindua mashindano ya michezo ya Taifa CUP ambayo yalikuwa yafanyike zamani lakini yalikuwa kwa mchezo mmoja ama miwili, kutokana na umuhimu wa michezo hiyo Serikali imekusudia kufufua na kuiendeleza ili iweze kufikia malengo yake ya kuibua na kuendeleza vipaji vya michezo nchini hasa kwa kuwapa nafasi zaidi wanamichezo na wasanii walioko mikoani.
"Kwenye mashindano ya mwaka huu tunaanza na michezo mitatu ambayo ni soka kwa wanaume na wanawake, netiboli kwa wanawake, na riadha kwa wanaume na wanawake .Mashindano haya yamepangwa kuanza Desemba 10 hadi 16 mwaka huu katika viwanja vya Benjamin Mkapa, Uhuru na Uwanja wa Ndani wa Taifa, kwa yale mashindano ya sanaa tutaanza na muziki na yatafanyika hapo hapo Uwanja wa Mkapa,"amesema Bashungwa.
Ametumia nafasi hiyo kufafanua kuwa wapo wengine wanatamani michezo hiyo ishirikishe michezo mingi zaidi ya iliyotajwa ."Nawaomba mtuelewe na tushirikiane mwaka huu tuanzie hapo , bajeti za kuendeleza mashindano haya ni kubwa sana,nasi tutaongeza michezo zaidi kadri ya uwezo wetu."
PICHA ZAOTE NA MICHUZI JR-MMG
Meza kuu ikiongozwa na waziri Bashungwa wakizindua bodi ya mfuko wa utamaduni na sanaa, mfumo wa kidigitali wa BASATA , Mfumo wa kidigitali wa Bodi ya Filamu, Mfumo wa kidigitali wa COSOTA,mashindani ya Samia Taifa CUP mbele ya wadau na wageni waalikwa mbalimbali.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Tamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi akizungumza jambo na wadau wa sanaa
Wadau wakibadilishana mawazo ukumbini
Kabla ya Wageni wa Mezaa kuu kufika
Waziri wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa akiwa ameambatana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo wa Zanzibar Bi. Tabia Mwita walipokuwa wakiwasili ukumbini
Wageni waalikwa mbalimbali walifika kushuhudia tukio hilo adhimu
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Tanzania Bw.Yusuph Singo akizungumza kwenye uzinduzi wa Bodi ya Mfuko wa Utamaduni na Sanaa, Mifumo ya Kidigitali ya BASATA, Bodi ya Filamu na COSOTA na Mashindano ya Samia Taifa Cup, uliofanyika katika ukumbi wa JNICC Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Tanzania Bw.Yusuph Singo akizungumza kwenye uzinduzi wa Bodi ya Mfuko wa Utamaduni na Sanaa, Mifumo ya Kidigitali ya BASATA, Bodi ya Filamu na COSOTA na Mashindano ya Samia Taifa Cup, uliofanyika katika ukumbi wa JNICC leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo wa Zanzibar Mhe.. Tabia Mwita akiwatuza wasanii wa kikundi cha TaSUBa
Waziri Bashungwa na Katibu Mkuu Dkt Abbasi wakijimwaya mwaya kidogo na burudani ya ngoma kutoka kikundi cha TaSUBa
Kupongezwa kwa uchakavu pia ulikuwepo
Burudani murua kabisa ikitolewa na kikundi cha ngoma cha TaSUBa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Tamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi akizungumza kwenye uzinduzi wa Bodi ya Mfuko wa Utamaduni na Sanaa, Mifumo ya Kidigitali ya BASATA, Bodi ya Filamu na COSOTA na Mashindano ya Samia Taifa Cup, uliofanyika katika ukumbi wa JNICC leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Tamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Pauline Gekul akizungumza kwenye uzinduzi wa Bodi ya Mfuko wa Utamaduni na Sanaa, Mifumo ya Kidigitali ya BASATA, Bodi ya Filamu na COSOTA na Mashindano ya Samia Taifa Cup, uliofanyika katika ukumbi wa JNICC leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo wa Zanzibar Mhe.. Tabia Mwita kwenye uzinduzi wa Bodi ya Mfuko wa Utamaduni na Sanaa, Mifumo ya Kidigitali ya BASATA, Bodi ya Filamu na COSOTA na Mashindano ya Samia Taifa Cup, uliofanyika katika ukumbi wa JNICC leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Tamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Innocent Bashungwa akizungumza kwenye uzinduzi wa Bodi ya Mfuko wa Utamaduni na Sanaa, Mifumo ya Kidigitali ya BASATA, Bodi ya Filamu na COSOTA na Mashindano ya Samia Taifa Cup, uliofanyika katika ukumbi wa JNICC leo Jijini Dar es Salaam.
Msanii wa Kizazi Kipya Saraphina akitoa burudani kwenye uzinduzi wa Bodi ya Mfuko wa Utamaduni na Sanaa, Mifumo ya Kidigitali ya BASATA, Bodi ya Filamu na COSOTA na Mashindano ya Samia Taifa Cup, uliofanyika katika ukumbi wa JNICC leo Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Dkt Abbasi akisalimiana na Msanii wa Bongofleva Yound D
Maelekezo Kidogo

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...