JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kesho tarehe 10 Novemba, 2021 anatarajiwa kuondoka nchini kuelekea Cairo nchini Misri kwa ziara ya Kiserikali ya siku tatu.
Ziara hiyo ya Kiserikali ya siku tatu inafuatia mwaliko wa Rais wa nchi hiyo, Mhe. Abdel Fattah Al Sisi.
Katika ziara hiyo, Mhe. Rais Samia pamoja na mambo mengine anatarajiwa kufanya mazungumzo na mwenyeji wake katika maeneo kadhaa ya ushirikiano kati ya Tanzania na Misri ikiwemo nyanja za diplomasia, uchumi, siasa, elimu, utalii na huduma za kijamii.
Mhe. Rais Samia na mwenyeji wake pia wanatarajiwa kushuhudia utiaji saini mkataba mmoja (1) na hati saba (7) za makubaliano kati ya Tanzania na Misri.
Jaffar Haniu
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...