Na Amiri Kilagalila,Njombe
Kutokana na matumizi makubwa ya Tehama na kuendelea kukua kwa uchumi nchini,serikali imesema inatarajia kuanzisha mafunzo ya Tehama yatakayosimamiwa na VETA katika wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe.
Hayo yamebainishwa na naibu waziri wa elimu sayansi na teknolojia Omary Kipanga wakati akikagua hali ya miundombinu ya majengo ambayo yaliachwa na kampuni ya kichina ya CHICCO iliyokuwa ikijenga barabara ya Nyigo-Igawa katika kijiji cha Soliwaya wilayani humo na kukabidhiwa mamlaka ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi (VETA) kanda ya Iringa kwa ajili ya kufungua chuo cha ufundi.
“Maagizo ambayo tumewapa VETA hapa ni angalau tuanze zile kozi ambazo hazihitaji karakana kubwa,kwa hiyo tutaanza na kozi ya umeme,uwashi,ushonaji lakini kama mnavofahama Tanzania imekwenda kwenye uchumi wa Katina matumizi ya Teahama ni makubwa sana kwa hiyo tumewaambia hapa waanzishe kozi ya Kompyuta pamoja na tehama.Hizo ndio kozi zitakazo anza wakati tunahakikisha tunakuwa na karakana ya zile kozi zinazohitaji uwepo wa karakana na mitambo”alisema Omary Kipanga
Aidha Kipanga amesema hali ya miundombinu ambayo imeanza kuchakaa tangu wachina hao kuikabidhi veta miaka miwili iliyopita,serikali imeidhinisha kiasi cha shilingi milioni 325 ili kianze kukarabati majengo hayo.
“Na maagizo yetu sasa tulichoagiza ndani ya miezi ya tatu ukarabati uwe umekamilika na tunatarajia kama mambo yatakwenda vizuri mpaka kufika mwakani mwezi wa tatu ukarabati utakuwa umekamilika na vijana wetu wataanza mafunzo hapa”aliongeza Kipanga
Mbunge wa jimbo la wanging'ombe ambaye ni Naibu waziri TAMISEMI Dkt.Festo Dugange amesema sasa watoto wanaokwama kuendelea na masomo ya Secondari watapata nafasi ya kuendelea na masomo ya ufundi ikiwa ni moja ya kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira nchini.
“Haya majengo yamekaa kwa takribani huu mwaka wa tatu na wilaya yetu hii haina VETA,na tuliomba yaanze kutumika kwa wanafunzi wetu wale ambao hawahitaji sana mitambo kwasababu karibu kila kitu hapa kipo”alisema Dugange
Baadhi ya wakazi wa kata hiyo akiwemo Golden Mbata na Jane Kisakanike wameshukuru kwa hatua ya serikali kuruhusu eneo hilo likarabatiwe ili chuo kifunguliwe na kuanza kutoa mafunzo kwa watoto wao.
Kwa hatua ya awali serikali imepanga kuanza kutoa mbali mbali ikiwemo za kompyuta na tehema kuanzia mwezi Machi mwakani chuo kitakapofunguliwa.
Naibu waziri wa elimu sayansi na teknolojia Omary Kipanga akizungumza na viongozi wa wilaya mara baada ya kukagua majengo ya VETA wilayani Wanging’ombe.
Mbunge wa jimbo la Wanging’ombe Dkt,Festo Dugange akimtembeza kwenye majengo ya VETA yaliyopo katika eneo hilo naibu waziri wa elimu sayansi na teknolojia Omary Kipanga alipofika na kukagua majengo hayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...