Pamela Mollel Arusha,

Katika kuzuia na kupambana na magonjwa yanayovuka mipaka,serikali kupitia ofisi ya waziri Mkuu imeanza kuratibu zoezi la kudhibiti magonjwa hayo ili kuhakikisha yanadhibitiwa pindi yanapojitokeza ili kuepusha kusambaa zaidi

Akizungumza Katika kikao kazi Cha kupitia na kuhakiki afya ya pamoja kinachojulikana kama Afya moja kwa Kanda ya Afrika Mashariki kilichowakutanisha wataalamu wa Afya za wanyama,wanadamu na mazingira Naibu Katibu Mkuu kutoka ofisi ya waziri Mkuu anaesimamia Sera, uratibu wa shughuli za serikali na bunge Kasper Muya amesema lengo la mkakati huu ni kutafuta jinsi ya kudhibiti magonjwa yanayovuka mipaka hususan yanayotoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu

Aidha amesema changamoto kubwa kwa Sasa ni kuibuka kwa magonjwa yanayosambaa kwa haraka hivyo Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia idara ya maafa wamekutana ili kuona ni kwa namna gani watadhibiti magonjwa hayo

"Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikisha na wataalamu wa idara zote za afya hususan wanaohusika na vimelea tumekutana ili tuweke nguvu ya pamoja kwa kuyadhibiti haya magonjwa"Alifafanua

Naye mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani WHO Daktari Grace Saguti amesema kikao hicho kitaishirikisha jamii kuanzia ngazi ya chini ili wajue jinsi magonjwa yanayosambaa kwa kasi yanavyovuka mpaka

Washiriki katika kikao hiki akiwemo Daktari Khadija Omary kutoka Wizara ya Kilimo,umwagiliaji,maliasili na mifugo Zanzibar wanasema wamekutana kuhakikisha katika ukanda wa Afrika Mashariki kunakuwa na mkakati wa pamoja katika kuzuia magonjwa hayo yanayovuka mipaka

Kikao hiki Cha siku tatu kimeratibiwa na ofisi ya waziri Mkuu idara ya Maafa kikile nga katika kuhakikisha ukanda wa Afrika Mashariki wanazuia pamoja na kupambana na magonjwa yanayovuka mipaka,hususan magonjwa ya mlipuko ukiwemo ugonjwa wa UVIKO 19.
Walaamu wa Afya kutoka  idara mbalimbali za Afya  waliokutana kwa pamoja kujadili namna ya kudhibiti magonjwa ya mlipupo wakiwa Katika picha ya pamoja jijini Arusha
Naibu Katibu mkuu kutoka ofisi ya Waziri mkuu Kasper Muya kulia akiteta jambo na Daktari Khadija Omary kutoka Wizara ya kilimo,umwagiliaji,maliasili na mifugo Zanzibar


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...