Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amesema kwa kuwa suala la uraia pacha linahitaji mchakato wa kikatiba kwasasa wataanza utaratibu wa utoaji wa hadhi maalumu (special Status) kwa Watanzania wanaoishi ughaibuni.
Balozi Mulamula ameyasema hayo leo Jumamosi Novemba 20, 2021 wakati akizungumzia mafanikio ya miaka 60 ya uhuru wa Tanzania Bara ndani ya Wizara hiyo
"Tunaondoka kwenye uraia pacha tunaingia katika hati maalum ambayo tunaona kuwa itatuvusha. Kama unavyojua uraia pacha ni mchakato wa kikatiba,” - Waziri Balozi Mulamula
Balozi Mulamula amesema amesoma na kuelewa utaratibu wa utoaji wa hati maalum unaotumika katika nchi nyingine ikiwemo India ambao ndio njia mbadala ya kuweza kutambua mchango wao na haki ambayo wamekuwa hawapati katoka kipindi hiki.
Aidha, Balozi Mulamula ameeleza kuwa mwaka 1962 mara baada ya uhuru kupatikana walikuwa na balozi mbili tu katika nchi za Uingereza na Umoja wa Mataifa nchini Marekani lakini hadi sasa wanabalozi 44 na balozi ndogo sita.
WAZIRI Mulamula pia Amesema hivi karibuni wakati wa Serikali ya Awamu ya Sita wamefungua Balozi ya Vienna na baadaye watafungua Jakata nchini Indonesia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...