Wahitimu Sekele Mwakisegile(Kushoto) na Clonerius Mwesiga(Kulia) wakisoma shairi wakati wa mahafali hayo katika shule ya awali na msingi ya Bwawani "Universal Pre and Primary School" iliyopo Kata ya Ubena Kijiji Cha Visakazi Wilaya ya Bagamoyo Halmashauri ya Chalinze Mkoani Pwani.
Na Khadija Kalili, Chalinze
Afisa Elimu wa Shule ya Msingi katika Halmashauri ya Chalinze Mkoa wa Pwani Miriam Kihiyo ameahidi kutatua Changamoto ya ukosefu wa maji na umeme katika shule ya awali na msingi ya Bwawani "Universal Pre and Primary School" iliyopo Kata ya Ubena Kijiji Cha Visakazi Wilaya ya Bagamoyo Halmashauri ya Chalinze Mkoani Pwani.
Kihiyo alisema hayo alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali ya Sita ya wanafunzi waliokuwa wamehitimu kuanza darasa la kwanza mwakani shuleni hapo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki.
"Naomba wazazi tusimamie maadili na nidhamu kwa watoto wetu nidhamu za watoto wetu zianzie majumbani katika ngazi ya familia ikiwa ni pamoja na kuvaa mavazi yenye kustiri maungo yao na yenye nidhamu, pitieni madaftari ya watoto pindi wanaporudi kutoka shuleni msiwaachie mzigo huo waalimu peke yao" alisema Kihiyo.
Akizungumza kuhusu changamoto ya ukosefu wa maji na umeme shuleni hapo aliahidi kylisimamia jambo hilo na kugakikisha huduma hiyo muhimu inawafikia katika eneo shuleni hapo huku alisisitiza kwa kusema kuwa ataongea na Wizara ya Ardhi ili wahusika watafutwe wa meeneo taliyoachwa na kuwa pori linalozunguka eneo la Shule Hali inayotoshia usalama wa wanafunzi na waalimu kwa ujumla Ili wahusika waweze kupunguza mapori hayo.
Naye Meneja wa Shule hiyo Mary Clara Daniel alisema kuwa kuwa Shule hiyo ilianzishwa mwaka 2016 ambapo kwa Sasa ina wanafunzi 132 huku wanafunzi waliohitimu ni 23 ambapo wasichana 12 na wavulana 11.
Akizungumzia kwa upande wa taaluma shuleni hapo alisema kuwa wako vizuri sana kitakwimu ni ya 145 kitaifa, pia imeshika nafasi ya sita kimkoa na katika mtihani wa darasa la nne wameshika nafasi ya nne katika ngazi ya Wilaya .
Meneja huyo wa Shule alisema kuwa wanaunga mkono jitihada za serikali katika kufuta ujinga huku wanafunzi wa shule hiyo wakitoka katika maeneo ya Mikese na Mdaula huku mipango ikipangwa ya kufuata watoto kutoka Lugoba na Morogoro.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...