Na Damian Kunambi, Njombe
Mahakama ya wilaya ya Ludewa iliyopo mkoani Njombe imemhukumu kifungo cha maisha jela George Lupindu(19) mkazi wa kijiji cha Ngalawale kwa kosa la kumbaka mtoto wakike mwenye umri wa miaka 9.
Akisomewa hukumu hiyo na hakimu Isaack Ayengo katika shauri namba 37/2021 Geaorge Lupindu ametiwa hatiani kwa kosa la ubakaji kinyume na kifungu cha 130(1)(2)(e) na 131(3) cha Kanuni ya Adhabu, Sura namba 16 ya Sheria za Tanzania kama ilivyofanyiwa Mapitio mwaka 2019.
Imeelezwa na Mwendesha Mashtaka Asifiwe Asigile kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo mnamo Julai 7 mwaka huu ambapo anadaiwa kumrubuni mtoto huyo (jina limehifadhiwa) wakati akitokea shuleni kwa kumdanganya kuwa anampeleka nyumbani kwao na kisha kumkamata kwa nguvu na kutenda kosa hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...