Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo imetangaza kuzindua kampeni ya kuweka akiba – “Kuza Akiba Ushinde na Timiza Akiba” ambapo wateja wa Airtel Money watapata fursa ya kushinda hadi Tzs20, 000 kila wiki pale wanapoweka akiba kwenye akaunti ya Timiza Akiba na bila kutoa kwa wiki hiyo.
Timiza Akiba ambayo ni akiba ambayo inapatikana kwa simu za mkononi kwa wateja wote wa Airtel Money, ni rahisi kutumia na inatoa riba kwa kila mwezi kwa kila anayewekeza. Riba hii hutolewa kulingana na kiasi kilichopo kwenye akaunti ya Timiza Akiba na hutolewa kwa lengo la kuhamasisha Watanzania kujenga utamanduni wa kujiwekea akiba.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kutangaza kuzindua kampeini hiyo ya Kuza Akiba Ushinde na Timiza Akiba, Mkurugenzi wa Airtel Money Isaack Nchunda alisema, ‘Kampeni hii ina lengo la kuhamashisha utamanduni wa kuweka akiba kwa wateja wa Timiza Akiba na vile vile kuwavutia wateja wengine wapya. Tunaendelea kutoa wito kwa Watanzania kuendelea kujenga utamanduni wa kuweka akiba alisema Nchunda huku akiongeza kuwa Airtel Tanzania imeshirikiana na Letshego Bank kuendesha kampeni hii”.
Nchunda aliongeza, ‘Lengo letu ni kuwahimiza wateja wetu waendelee kuweka akiba Zaidi kwenye akaunti zao za Timiza Akiba kupitia Airtel Money na kwa wateja wapya kufungua akaunti na kuanza kuweka akiba kwenye Timiza Akiba ili kupata nafasi ya kushinda hadi Tzs20,000 kila wiki.
Akizungumzia jinsi washindi watakapokuwa wanapatikana, Nchunda alisema kuwa mteja yeyote wa Airtel Money anayeweka kiasi cha Tzs20,000 kwa wiki kwenye akaunti ya Timiza Akiba atakuwa na nafasi ya kuingia kwenye droo na kushinda mara moja kwa wiki.
Aliongeza, ‘Washindi 25 watakuwa wakipatakana kila wiki kupitia droo itakayokuwa ikiendeshwa na Airtel katika wiki sita za kampeni hii. Washindi hao watapata zawadi zao za Tzs20,000 kila mmoja kupitia akaunti zao za Airtel Money.
“Nachukua nafasi hii kuwaomba wateja wa Airtel Money na vile vile wale ambao sio wateja wa Airtel Money kutumia fursa hii na kuanza kuwekeza kupitia Timiza Akiba na kushindia Tzs20, 000 kila wiki. Wateja hawahitaji kujisajili au kulipa chochote kupata fursa ya kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kushinda,’ alisema Nchunda.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Letshego Benki Tanzania, Bw, Omar Msangi alisema kuwa wao kama benki wameamua kushirikiana na Airtel kuendesha kampeni hiyo ili kuungana mkono jitihada za kuleta suluhisho la huduma za kifedha hapa nchini pamoja na kuendelea kujenga utamanduni wa kuweka akiba kwa Watanzania. “Tunatoa rai kwa Watanzania kuendelea kujenga utamanduni wa kujiwekea akiba kwa matumizi ya baadae. Pia naomba niwaakikishie kuwa washindi wote watapata zao kupitia akaunti zao za Airtel Money”.
Aliongeza, “Timiza Akiba ni matokeo ya chanya ya kushirikiana na Airtel ambayo inaonyesha jinsi Letshego ilivyojipanga kuinua maisha. Ushirikiano huu kwetu unabaki kuwa ni nyenzo muhimu sana kwetu pamoja na Airtel, tutaendelea kuwaamasisha Watanzania waendelee kuwejenga utamanduni wa kujiwekea akiba kidigitali popote pale walipo.
Mkurugenzi wa Airtel Money Tanzania, Isaack Nchunda (kulia), akigongeshana mkono na Mkurugenzi wa benki ya Letshego, Omar Msangi, wakati wa uzinduzi wa kampeini ya Kuza Akiba Ushinde na Timiza Akiba iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi wa benki hiyo, Simon Jengo.
Mkurugenzi wa Airtel Money Tanzania, Isack Nchunda (kulia), akigongeshana mkono na Mwenyekiti wa Bodi wa benki Letshego, Simon Jengo (katikati). Wakati wa uzinduzi wa huduma ya Kuza Akiba Ushinde na Timiza Akiba iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo, Omar Msangi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...