Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva na R&B Behman Paul ‘Ben Pol’ amejiandaa kufunga mwaka 2021 na mashabiki sambamba na kupata chakula cha jioni pamoja.

Katika hafla hiyo, Ben Pol ameweka wazi kuwa anataka kufunga mwaka na mashabiki wake na kufurahia pamoja sambamba na kuwapa burudani ya muziki.

Ben Pol anatarajia kuuaga mwaka 2021 na kuukaribisha mwaka 2022 kwa staili ya show kubwa ya Muziki wa Live ambayo itaambatana urushaji wa Mafataki kuukaribisha Mwaka mpya 2022.

Show hiyo inatarajiwa kufanyika Katika mkesha wa mwaka mpya Desemba 31, ambapo ataanza kwa kujumuika katika chakula cha jioni pamoja na mashabiki zake watakaohudhuria usiku huo, pia kutakuwa na michezo ya watoto, na muziki wa live ukiongozwa na Ben Pol na bendi yake.

“Mashabiki zangu wamekuwa wakizipokea vizuri sana kazi zangu kwa muda mrefu sasa, Nashukuru kwa upendo na support kubwa wanayonipa, nina kila sababu ya kusherehekea kwa kujumuika nao kwa chakula na muziki mzuri wa live kwenye mkesha wa mwaka mpya,” amesema

Ben Pol amesema, asilimia 20 ya mapato nitakayopata kwenye usiku huu nimepanga kuyarudisha kwa jamii kwa kuwasaidia vifaa vya shule wanafunzi wanaoanza shule ya msingi mwaka 2022 waishio kwenye mazingira magumu” Amesema Mkali wa R’nB Behnam a.k.a Ben Pol.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...