NA FARIDA SAIDY, MOROGORO.

Mkurugenzi msaidizi huduma za ustawi wa jamii kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) RASHEED MAFTAH amewaagiza waratibu wa mikoa wa mfuko wa afya ya jamii ulioboreshwa (CHF) kwenda kusimamia fedha zilizotolewa na serikali kwa kushirikiana na wadau kwa ajili ya kuwapatia bima ya afya ya (CHF) kwa watoto wanaotoka katika mazingira hatarishi

Akizungumza na waratibu hao wakati wa kuwajengea uwezo wa ukusanyaji wa fedha za mfuko wa CHF kwa njia ya kieletroniki Bw. MAFTAH amesema fedha Bilion 4.6 zimetolewa na serikali kwa ajili ya kuborasha upatikanaji wa bima za afya kwa Watoto walio katika mazingira hatarishi.

Katika warsha hiyo wamepatiwa mafunzo ya matumizi ya kukusanya fedha kwa njia ya kieletroniki kwa mfuko afya ya jamii ulioboreshwa CHF ambapo mada mbalimbali zimewasilishwa pamoja na namna ya mfumo huo unavyofanya kazi.

Katika hatua nyingine ameleza lengo la kuanzishwa kwa mfumo huo ni kukusanya fedha za umma, kutatua changamoto pamoja na kuongeza udhibiti wa upotevu wa fedha za umma na kuleta imani kwa wanachama kuhusu michango yao iliyokusanywa.

Kwa upande wake mratibu wa (CHF) SILVERY MAGANZA ameeleza kuwa mfuko huo ulianzishwa rasmi Juni, 2018 ambapo mfuko huo kwa sasa umekuwa tegemezi kwa wananchi huku akisema jumla ya shilingi 25.5 bilioni zimekusanywa kwa ajili ya mfuko huo.

Nae SELLA BAGIRA ambaye ni msimamizi wa mawasiliano wa maduka ya dawa za binadamu (pharmacy) ambao ni wadau katika kuendeleza mfuko amewaomba washiriki wa mafunzo hayo kwenda kutekeleza yale waliopatiwa mafunzo kwa uwaandaji na ukusanyaji wa mapato kwa kutumia njia ya kieletroniki.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...