Na Ashura Mohamed,Arusha

Katibu mkuu wa wizara ya Afya Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dokta John Jingu amewataka maafisa maendeleo ya jamii nchini kujikita zaidi katika utatuzi wa changamoto zinazoikabili jamii,hususani katika maeneo ya vijijini kwani kuna changamoto nyingi ambazo hazijatatuliwa.

Katibu mkuu ameyasema hayo katika mahafali ya 12 ya wahitimu wa chuo cha maendeleo ya jamii Monduli ambapo jumla ya wanafunzi 539 walihitimu kozi ya Astashahada ya Awali ya Maendeleo ya Jamii na Stashahada .

Alisema kuwa Maafisa hao wana wajibu mkubwa wa kutatua changamoto katika jamii hususani kukemea mila ambazo,zimepitwa na wakati kwani wana uwezo mkubwa wa kuibadili jamii na kuweza kuachana na fikra potofu ili waweze kuendana na mtazamo wa kisasa .

"Nyie ndo mnatakiwa kuja na mwarobaini na kutatua changamoto katika jamii hususani vijijini,kwani bado jamii inakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinawahitaji mfike na kuweza kuja na mwarobaini ,hivyo hakikisheni mnaitumia vyema elimu mliyoipata kunufaisha jamii"Alisema Jingu

Hata hivyo ametaka kuendelezwa kwa programu ya uanagenzi kwenye vyuo mbalimbali kwani zinasaidia kujenga uwezo wa kujiajiri kwa wanafunzi na kuweza kuondokana na changamoto ya ajira.

Mkuu wa chuo cha Maendeleo ya Jamii Monduli bw.Elibariki Ulomi alisema kuwa,Chuo hicho kimekuwa kikitoa elimu juu ya ukatili wa kijinsia katika jamii na hata mashuleni na kuweza kuwajengea uelewa juu ya hatua za kuchukua pindi wanapogundua kuwepo kwa ukatili huo.

Alisema kuwa wameendelea kutekeleza maagizo mbalimbali ya wizara ikiwa ni pamoja na kushughulikia masuala ya ubunifu na maarifa,uanagenzi ushirikishwaji jamii,pamoja na uboreshaji wa makazi ya wanajamii .

"Kwa kushirikiana na wananachi wa Kijiji Cha Eluway kilichoko kata ya Monduli juu,tunashughulikia changamoto ya kukosekana kwa maji katika zahanati ya Kijiji cha Eluway,ambapo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali tumeweza kufanikisha mradi huo wa uvunaji wa maji ya mvua ambapo umegharimu shs 6.4 milioni"alisema .

Naye Mmoja wa wahitimu aliyehitimu chuoni hapo na kuibuka mwanafunzi bora wa kuandika tafiti iliyolenga maswala ya Afya,Noel Makuu alisema kuwa anashukuru namna ambavyo chuo hicho kilivyomwandaa na kuweza kufanya utafiti na kujua ni sababu gani inayopelekea wanaume kutoshiriki huduma za afya na wake zao wilayani Monduli ambapo tafiti zimeonesha kuwa wanaume wengi wana upungufu wa elimu,pamoja na mila potofu zilizopo katika jamii ya wafugaji ambapo wanaume wengi wanaona kuwa watadharaulika endapo wataongozana na wake zao kupata huduma za uzazi,hivyo elimu bado inahitajika kwa kiwango kikubwa.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...