waandaaji na wadhamini wa Familia Marathon 2021 wakionyesha kwa waandishi habari, Dar es Salaam leo, medani na baadhi ya zawadi watakazopewa washiriki wa mbio hizo zitakazofanyika kwa mtindo wa kutembea na kukimbia jijini humo jumamosi wiki hii. Mbio za mwaka huu zimedhaminiwa na  KCB Bank, KP Motors, UTT Amis, Premier Security, Optical Centre, Rani Sanitary Pads, Planet Fitness, Knight Support na Xpress Rent.
Meneja wa Kampuni ya Rani Sanitary Pads, Mawi Zahor  (kulia ), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu udhamini wao katika mbio za Familia Marathon 2021 zinazotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam jumamosi wiki hii.

Mkurugenzi Uendeshaji wa Planet Fitness, Ramadhani Mdula (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu udhamini wao katika mbio za Familia Marathon 2021 zinazotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam jumamosi wiki hii.

 

Mkurugenzi Mtendaji was Kampuni ya magari ya KP Motors, Anita Kisima (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu udhamini wao katika mbio za Familia Marathon 2021 zinazotarajiwa kutimua vumbi lake jijini Dar es Salaam jumamosi wiki hii. KP Motors itatoa zawadi ya gari  aina ya Passo mpya kwa mshindi mwanamke kati ya washindi kumi atakayeshinda mbio za KM 21. Kushoto kwake ni Mkuu wa Masoko Mawasiliano na Uhusiano wa Benki ya KCB, Christina Manyenye na Ofisa Masoko wa UTT Amis, Rahim Mwanga.
Ofisa Habari Familia Marathon (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam Disemba 11, jumamosi. Mbio zitaanzia Msasani Beach Club kuanzia saa 12 asubuhi zikijumuisha mbio za 21km -half marathon, 10km- Corporate Run na 5km -Social Run.

Mkuu wa Masoko, Mawasiliano na Uhusiano wa Benki ya KCB, Christina Manyenye (wa nne kushoto), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu udhamini wao katika mbio za Familia Marathon 2021 zinazotarajiwa kutimua vumbi lake jijini Dar es Salaam jumamosi wiki hii. Usajili unaendelea kufanyika katika Tawi la KCB Mlimani City. 
Mwenyekiti wa mbio za Familia Marathon 2021, Bi. Francisca Alphonce (wa tatu Kulia), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam Disemba 11, jumamosi. Wengine ni wawakilishi wa Kampuni zinazodhamini mbio hizo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...