Na Amiri Kilagalila

Ikiwa ni siku chache zimepita baada ya polisi mkoa wa Njombe kutangaza kupatikana kwa baadhi ya viungo vya mwili wa mtu alietambulika kuwa ni mfanyibiashara wa vitunguu ambae ni mkazi wa Morogoro, ndugu wa mfanyabiashara huyo wamefika na kulazimika kufukua mwili wa ndugu yao na kuusafirisha kwenda kuuzika nyumbani kwao.

Mfanyibiashara huyo ametambulika kwa jina la Jackson Charles ambaye ni mkazi wa Kilosa mkoani morogoro kwa mujibu wa nduguze, anaripotiwa kupotea tangu octoba 22 mwaka huu huko wilayani wanging’ombe mkoani na baadae baadhi ya viungo vya mwili wake vilipatikana katika msitu wa ngaramaro kijiji cha mtapa wilayani humo.

Kwa mujibu wa uongozi wa kata ya kidugala wilayani wanging’ombe ambako marehemu alikuwa anafanyia biashara mwili wa mfanya biashara huyo ulikutwa katika msitu ukiwa umeharibika na baaadhi ya viungo vikiwa havipo na ndipo serikali ikachukua jukumu la kuuzika siku ya desemba 5 mwaka huu

“Tulipata taarifa kuwa kuna mfanyabiashara alikuja kwenye kata hii lakini baada ya muda kidogo tulikuja kupata taarifa kwamba kuna mwili uko porini tukaenda tukijiridhisha lakini pia ule mwili ulikuwa umeharibika sana na viungo naadhi havikuwepo na kwasababu kulikuwa hakukuwa na tukio kwenye kata yangu kwamba kuna mtu amepotea basi mwili ule ukazikwa eneo lile lile”alisema Boston Vahaye mtendaji wa kata ya kidugala wanging’ombe

Ndugu na wafanyabiashara wenzake wa vitunguu kutoka jijini Dar es salaam wamefika kuuhamisha mwili huo katika eneo la msitu huo wakiwa katika hali ya majonzi mazito.

“Huyu ni mototo wa watu na anategemewa na familia yake leo hii ankuja kuzikwa kinyama kama mbwa hapa miguu na mikono yote wamekata,huu ni unyama kabisa”alisema Matrida gregory ,mfanyabiashara.

Siku chache tu zimepita baada ya Kamanda wa polisi mkoa wa njombe Hamiss Issa kuthibitisha juu ya tukio hilo na kuutangazia umma na kuthibitisha kushikiliwa kwa mtuhumiwa mmoja kutokana na tukio hilo.

“Na bahati nzuri Yule aliyekuwa naye kweli amekiri kuhusika na mambo yaliyopelekea mpaka huyu amefariki na fedha aliyokuwa nayo waliichukua “alisema Hamis issa kamanda wa polisi mkoa wa njombe wakati akitangaza tukio hilo

Bado polisi mkoa wa njmbeinaendelea na uchunguzi wa kina kubaini wote wanojihusishanamatukio ya uhalifu ikiwemo uporaji wizi na ubakaji.

Viungo vya mwili wa marehemu vikiwekwa kwenye jeneza mara baada ya kufukuliwa kwa ajili ya kusafirishwa.

Baadhi ya ndugu wa marehemu na wafanyabiashara wakiufukua mwili wa ndugu yao uliozikwa ardhini mara baada ya kutambuliwa


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...