Na Khadija Kalili, Kibaha
Katibu wa Chama Cha Wafanyakazi wa Vyombo Vya Habari Tanzania (JOWU TA) Suleiman Msuya ametoa hamasa kwa Waandishi wa habari kujiunga na Chama hicho ambacho ni chama huru kwa wanahabari wote nchini Ili waweze kutetea haki zao za msingi ambazo zimepokwa kwa miaka mingi na vyombo mbalimbali ambavyo wamekua wakivitumukia.
"JOWUTA ambacho Mwenyekiti wake wa Taifa ni Claudio Gwangu ni sehemu sahihi kwa wanahabari katika kutetea maslahi yao kwani haina masharti magumu ya kujiunga ambapo pia taasisi hii imekuja katika wakati muafaka hivyo wanahabari tuchangamkie fursa za kujiunga" alisema Msuya.
Katibu huyo wa JOWUTA aliyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya siku mbili kwa Waandishi wa habari yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Njuweni Kibaha huku akise kuwa tayari mafunzo kama haya yameshafanyika kwenye mikoa 16 nchini na yameweza kuamsha ari ya wanahabari wengi kujiunga na JOWUTA.
Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Pwani Ally Hengo alisema kuwa amefurahi kupata fursa hiyo ya mafunzo kwa wanachana wake miongoni na kuchagiza hamasa ya kujiunga kwani wao ndiyo walengwa wa changamoto zote wanazozipitia wanahabari.
Hengo amewashukuru JOWUTA na kusema kuwa anaunga mkono juhudi zao na kwamba atahakikisha anatoa hamasa ya kutosha kwa wanahabari wengine wa Mkoa wa Pwani kujiunga na Taasisi hiyo.
"Sisi wanahabari tunapaswa tujisemee wenyewe Sasa katika kudai haki zetu na kujijenga kwani tumekua daraja na kuwachongea Taasisi mbalimbali kujipigania maendeleo huku sisi tukijisahau na tukikosa sauti moja ya kijisemea"alisema Hengo.
Mafunzo hayo ya siku mbili yalijikita katika kutoa elimu ya usalama masalama mahala pa kazi n usawa wa kijinsia yamedhaminiwa na Chama Cha Wafanyakazi Cha Wanahabari wa Norway(NORSK LAG).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...