Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt. Amos Nungu akitembelea sehemu za kazi za ugunduzi za wanasayansi vijana kutoka shule za sekondari mbalimbali hapa nchini.

Na Mwandishi wetu, Globu ya Jamii
KATIKA kuhakikisha Wanasayansi Vijana wanafikia Malengo yao serikali ipotayari kutoa miundombinu rahisi wa wanasayansi hao.

Serikali inachukulia masuala ya kisayansi kwa umakini mkubwa ili kuhakikisha YST wanakuwa na ujunzi pamoja na kufuata maswali yote na misingi ya kisayansi.

Hayo yamesemwa na Mwakilishi wa Waziri wa Elimu na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt. Amos Nungu wakati wa kutoa zawadi kwa wanasayansi vijana kutoka shule mbalimbali za sekondari Nchini, amesema kuwa vijana hao wanapatikana kupitia walimu wao na shule wanazosoma.

Amesema kuwa wanajivunia kuwa na wanasayansi vijana kwani ndio wataokuwa wanasayansi wakubwa baadae.

Amesema kuwa wanasayansi vijana wamepitia njia zote za kutatua changamoto katika jamii kulingana na kile walichoonesha kwenye maonesho.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wanasayansi Vijana Tanzania (YST)na Profesa Yunus Mgaya amesema kuwa mashindano hayo wanaangalia ubora wa ubunifu wao na hawaangalii we ametokea kwenye jamii gani na mawazo yao yanawezaje kutatua changamoto zilizopo shuleni kwao au matatizo yaliyopo kwenye jamii.

Amesema wanamiradi mbalimbali ya kisayansi ikiwemwo Kemia, Fizikia, Bayolojia, mahesabu, Sayansi ya Kompyuta, Sayansi ya Mazingira na sayansi ya jamii.

Prof. Mgaya amesema kuwa wanashiriki kuwaongoza wanasayansi vijana na kuboresha vipaji vyao, akizungumzia kwanini YST hapa nchini ni kwaajili ya kuibua vipaji vya wanafunzi katika shule za sekondari kuanzia Kidato cha Kwanza hadi kidato cha Sita.

Amesema kuwa YST kwa wale wanaofanya vizuri zaidi wanapata ufadhili wa kusoma vyuo vikuu vya hapa nchini.

Amewaomba wadau kuwaunga mkono huku akiwashukuru wadau wanaounga mkono juhudi za YST na kuendelea kusonga mbele.

Kwaupande Afisa Mtendaji wa Karimjee Jivanjee Foundation, Caren Rowland amepongez juhudi za YST kwa kuanza na mikoa 10 tu na sasa wapo mikoa yote ya nchini.

Karimjee Jivanjee Foundation wanaunga mkono juhudi hizo na kuhakikisha Sayansi wanakuwepo hapa nchini pia wanatoa ufadhili kwa wanafunzi ambao wanafaulu vizuri masomo ya sayansi ili kukuza kipaji cha sayansi.

Mwanzilishi Mwenza wa shirikisho la Wanasayansi Chipukizi (Young Scientist Tanzania (YST)), Dkt. Gozbet Kamugisha amesema kazi za wanasayansi vijana 16 zimeoneshwa na zimewakilisha kazi 160 ambazo zinatatua matatizo katika jamii zetu.

"Sisi YST tunawaelekeza watumie sayansi wanaojifunza darasani kuitumia katika kufanya utfiti na kufanya ugunduzi wa Teknolojia ambazo zitamaliza matatizo yanayoikabilii jamii yao."

Amesema maonesho hayo yanaweza kuwasaidia vijana kukuza na kuweza kusoma katika utamaduni wa kufanya utafiti wakiwa bado wadogo.

"Samaki Mkunje angali mbichi, hawa samaki wetu bado wabichi wanakunjika kisayansi, tunategemea wanapokuwa watakuwa wanasayansi mahili na wavumbuzi wazuri." Amesema Dkt. Kamugisha

Kwa upande wa Mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya Nyihongo, Kahama Shinyanga Christina amesema wameshinda tuzo kutokana na kufanya utafiti juu ya faida za usingizi kwa mwanadamu.

Amesema kama mtu asipolala kwa masaa yanayotakiwa anaweza kupata tabia ambazo hazitarajiwi ikiwa ni kujisikia mchovu, kuumwa na kichwa kupata msongo, kupata hasira za mara kwa mara na kuwa na mihemko, na ikitokea Tabia hizi zimekuwa endelevu basi mtu anaweza kupata magonjwa ya yasiyoambukizwa kama ugonjwa wa moyo, figo, kisukari na mshtuko.

Anashauri kuwa binadamu anatakiwa kulala kuanzia masaa saba hadi nane hadi tisa kwa watoto wadogo, kwasababu watoto wadogo usingizi ni mhimu kwa ukuaji wao.

Amefafanua kuwa kwa mama mjamzito katika miezi tatu ya mwanzo wanahitaji isinginzi mwingi kuliko kawaida kwaajili ya afya yake pamoja na mtoto aliyetumboni.

"Usingizi unachukua Robo tatu ya maisha ya binadamu." Ameeleza Christina.

Mwanafunzi wa shule ya sekondari Mtwara Ufundi, Warda Mwanza akielezea athari za Unyago, Jando na athari za ndoa za utotoni amesema kuwa mafunzo ya jando na unyago yanasababisha wanafunzi kuacha shule kwasababu wakifika shule wanajiona kama wanapoteza muda na wanaacha shule.

Hivyo wanaishauri jamii kutokuwa na mila potofu zinazosababisha wanafunzi kuacha shule kwani elimu ni ukombozi.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt. Amos Nungu akizungumza wakati wa utoaji wa zawadi kwa wanasayansi vijana kutoka shule mbalimbali za sekondari Nchini, hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Kivukoni katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mshauri wa mahusiano wa kampuni ya Shell, Msomisi Mbenna akizungumza wakati wa hafla ya utoaji wa zawadi kwa wanasayansi vijana iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.


Mshauri wa mahusiano wa kampuni ya Shell, Msomisi Mbenna akipata maelezo wakati wa hafla ya kuwakabidhi zawadi wanasayansi vijana jijini Dar es Salaam.
Mshauri wa mahusiano wa kampuni ya Shell, Msomisi Mbenna akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanasayansi vijana katika hoteli ya serena jijini Dar es Salam.


Mwenyekiti wa Bodi ya Wanasayansi Vijana Tanzania (YST)na Profesa Yunus Mgaya akikabidhi zawadi kwa wanasayansi vijana katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji wa Karimjee Jivanjee Foundation, Caren Rowland akiwakabidhi wanasayansi vijana zawadi katika hafla iliyofanyika katika hoteli ya serena jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...