Bia ya Serengeti Lager leo
imewakutanisha uso kwa uso baadhi ya wachezaji wa Taifa Stars na
mashabiki katika hafla ya chakula cha jioni iliyofanyika jijini Mbeya
ikiwa ni muendelezo wa kampeni ya ‘Nje ya Dimba na Stars’
Kampeni
ya 'Nje ya Dimba na Stars' inalenga kuwapa nafasi mashabiki wa Taifa
Stars kukutana na nyota wanaowapenda katika baa zao na pia watapata
fursa ya kuwauliza maswali kuhusu maisha yao nje ya soka pamoja kupiga
nao picha za ukumbusho. Kampeni hiyo ya nchi nzima itadumu kwa miezi
mitatu.
Akiongea wakati wa hafla hiyo, meneja masoko wa kanda za
juu kusinini wa SBL Denis Tairo alisema bai ya Serengeti lager ikiwa
kama shabiki mkuu wa Taifa Stars inajivunia kuwaletea mashabiki wa Taifa
Stars mkoani Mbeya nyota inaowapenda na kuwapa nafasi kuzungumza nao na
hivyo kuwafahamu kwa undani zaidi.
“Shabiki mkuu na mdhamini wa
timu yetu ya taifa, Taifa Stars Bia ya Serengeti Lager leo
amewakutanisha mashabiki wa hapa Mbeya uso-kwa-uso na nyota ambao mara
nyingi wamekuwa wakiwaona uwanjani. Hii ni fursa pekee ya mashabiki
kujua maisha ya nota wao nje ya uwanjani,” alisema
Denis alisema
kampeni hiyo ya nchi nzima itahusisha wachezaji wa Taifa Stars ambapo
watatembelea mikoa ya Mbeya, Mwanza na Arusha na kukutana na mashabiki
wao kupitia matukio kama pati za mwisho wa mwezi ‘Nje ya Dimba na
Stars’. Kwenye matukio kama hayo mashabiki wataweza pia kujishindia
zawadi mbali mbali na ofa za bei yao pendwa ya Serengeti lager.
"Wachezaji
watakuwa kwenye baa mbali mbali na wakati wateja wetu wa bia ya
Serengeti Lager wakiendelea kuburudika na bia yao pendwa iliyotengenezwa
kwa kimea kwa asilimia 100 na isyoongezwa sukari, watapata nafasi ya
kuwauliza maswali, kupiga picha na kupata sahihi zao,” alisema
Aliwataka
mashabiki wa Stars kutembelea kurasa za mitandao ya kijamii ya bia ya
Serengeti Lager Pamoja na kusikiliza redio kwa ajili ya kujua linin a
wapi nyota wa taifa Stars watakuwa.
Meneja masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Denis Tairo (kati kati) akiwa na baadhi ya wachezaji wa Taifa Stars ikiwa ni muondelezo wa kampeni ya ‘Nje ya Dimba na Stars’ ambapo wachezaji hao walikutana uso kwa uso na mashabiki wao wa mkoa wa Mbeya.
Baadhi ya mashabiki wa Taifa Stars mkoani Mbeya wakiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu hiyo ya taifa, muda mfupi baada ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na bia ya Serengeti Lager ikiwa ni sehemu ya kampeni ya ‘Nje ya Dimba na Taifa Stars’
Mchezaji wa Taifa Stars Baraka Mwamunyeto, akijibu moja ya swali kutoka kwa mashabiki wa soka wakati wa tukio lililowakutanisha wacheza wa timu hiyo ya taifa na washabiki wao lililofanyika jijini Mbeya chini ya kampeni ya Nje ya Dimba na Stars inayoendeshwa na bia ya Serengeti Lager
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...