Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV
BAADA ya kuwepo kwa taarifa zinazodai uwepo wa taulo za kike zinazotengenezwa na Kampuni ya NN General Supplies inayotengeneza taulo za kike za HQ , uongozi wa kampuni hiyo umeamua kuzungumzia taarifa hizo na kueleza watafuatilia kujua ukweli.
Katika mitandao ya kijamii kumekuwepo na taarifa za maandshi na sauti ambazo zinadai Kampuni ya HQ ambayo imebobea katika utengenezaji wa taulo za kike,zikidai imegawa taulo zilizoisha muda wake kwa baadhi ya waandishi wa habari wanawake
Taarifa nyingine ambazo zipo kwenye sauti zilizorekodiwa na kusambazwa mitandaoni zinadai kuwa kampuni hiyo siku za karibuni imesambaza taulo za kike zilizoisha muda wake mashuleni.
Kutokana na taarifa hizo, Michuzi TV na Michuzi Blog iliona haja ya kumtafuta Mkurugenzi wa Kampuni ya NN General Supplies inayotengeneza taulo za kike za HQ Celina Letare ambaye ameeleza hatua kwa hatua kuhusu taarifa hizo ambazo amesema anazitilia shaka.
"Nimeona hii taarifa na watu kabla ya kuitoa wangenitafuta kama ulivyofanya wewe(Mwandishi),taulo sina uhakika kama zimeisha muda wake maana sikuwepo ,nina uhakika kuna kitu kimefanyika kwasababu sisi tulikuwa na jambo letu ile juzi.
"Hatujui hata zile taulo zimekwendaje pale lakini nitakuja kufuatilia nikirudi, kwa sasa niko nje ya nchi,lakini pia nafuatilia kwa karibu maana mtu anapotoa habari lazima awasiliane na wahusika,kuna subtarge za aina nyingi, kuna sauti nimesikia mtu akisema taulo tulizogawa mashuleni huenda zili-Expire lakini bahati nzuri taulo tulizogawa mashuleni tumegawa na Waziri na zipo na hakuna ambazo zime expire mashuleni,"amesema
Ameongeza kwamba kama kilichofanyika ni sabtarge ya mfanyakazi au wafanyakazi alitakiwa aambiwe ili akirudi ashughulikie.
Amesisitiza watalishughulikia suala hilo kwa mapana zaidi kwasababu wana uhakika na kazi wanayofanya."Mimi nafanya kazi na Mungu sifanyi kazi za kubabaisha, za kuumiza,hata kama zinge expire hazina madhara yoyote,zinaweza kukaa hata miaka mitatu lakini hakuna sababu ya kutoa kitu ambacho kime expire.
"Hivyo niwahakikishie nitakifanyia kazi nikirudi ,kwa sasa niko nje ya nchi, namuomba Mungu niirudi salama na nitashugulikia,nadhani kuna tatizo mahali.
Kwa mujibu wa taarifa zilizosambaa mtandaoni zinaeleza kuwa Desemba 8 mwaka huu mkoani Dar es Salaam ,Kampuni hiyo ilifanya mkutano na waandishi wa habari kwa lengo la kutangaza uboreshaji wa huduma za kampuni hiyo,sambamba na kugawa bidhaa hizo kwa waandishi waliokuepo katika mkutano huo.
Taarifa hizo zinaeleza katika hali ya kushangaza taulo hizo ziligundulikana kuwa zimeshakwisha muda wake wa matumizi kutokana na tarehe iliyopo katika taulo ambazo zilitolewa kwa waandishi wa habari.
Kuanza kusambaa kwa taarifa hizo kulianza baada ya mmoja wa waandishi kupiga picha mmoja ya taulo hizo na kisha kuirusha katika group ambalo lina waandishi na kuwataka kukagua, ndipo hapo sasa maswali na mijadala ikaibuka.
Hivyo Michuzi TV na Michuzi Blog ikaona kuna kila sababu za kuwatafuta viongozi wa Kampuni hiyo ili kupata majibu ya maswali mengi yaliyoibuka baada ya kuwepo kwa taarifa hizo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...