Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally (wa pili kulia) akiwa amesimama wakati Shirika lake la KIVULINI likitangazwa kushinda Tuzo ya Ruzuku kutokana na kuwa Kinara wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Shirika
la Kutetea haki za wanawake na Watoto - Kivulini lenye Makao yake Makuu
Jijini Mwanza limeshinda Tuzo ya Ruzuku kutokana na kuwa Kinara wa
Kupinga Ukatili wa Kijinsia hususani katika Kutokomeza Mimba za utotoni
na ndoa za utotoni na ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Shirika
la KIVULINI limepokea Tuzo hiyo Jumatano Desemba 8,2021 kwenye
Tamasha la Utoaji Tuzo kwa Mashirika sita Vinara wa Kupinga Ukatili wa
Kijinsia nchini Tanzania katika Siku 16 za Uanaharakati Kupinga Ukatili
wa Kijinsia‘A Joint Champions Award and Concert on 16 Days of
Activism Against Gender Based Violence – with over 30 artists, sports
champs and activists’ lililofanyika Serena Hotel jijini Dar es salaam.
Mashirika
sita yaliyotangazwa kuwa Vinara wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia likiwemo
Shirika la KIVULINI yatapokea mchango wa Fedha zilizokusanywa katika
tamasha hilo na mchango huo utaenda kusaidia jitihada zao za kupambana
dhidi ya ukatili wa kijinsia.
Tuzo
hizo za Ruzuku ambazo zimeing’arisha KIVULINI Kimataifa zimeandaliwa na
Taasisi za Umoja wa Mataifa ambazo ni UN Women, Shirika la Umoja wa
Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) pamoja na Umoja
wa Ulaya na Balozi mbalimbali nchini Tanzania ambazo zimetambua juhudi
zinazofanywa na Shirika la KIVULINI katika kutokomeza Mimba za utotoni
na ndoa za utotoni na ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Akizungumza
mara baada ya KIVULINI kutangazwa kuwa Shirika Kinara wa Kupinga
Ukatili wa Kijinsia nchini Tanzania, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la
KIVULINI, Yassin Ally amesema Tuzo hiyo ni ya haki kutokana na kazi
kubwa wanayoifanya katika kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia
hivyo wamefarijika kuona wapo watu wanatambua mchango wao na kuitangazia
dunia.
“Tunaushukuru
Umoja wa Ulaya na Taasisi za Umoja wa Ulaya na Balozi mbalimbali kwa
kutambua mchango mkubwa wa shirika la KIVULINI pamoja na mashirika
mengine matano kutoa Tuzo ya Kupambana na matukio ya ukatili wa
kijinsia. Hii kwetu sisi itatupa ari zaidi, nguvu kubwa kwa kwenda sasa
nyumba kwa nyumba, uvungu kwa uvungu na tutawekeza nguvu zaidi kwa
wananchi na taasisi za kiserikali ili kuhakikisha athari za ukatili wa
kijinsia hazinyamaziwi na kila mmoja anakuwa sehemu ya mabadiliko”,amesema Ally.
“Tuzo
hizi zimetutia moyo na kutupa thamani kubwa kwa sababu kazi
tunayoifanya inatambulika kitaifa na kimataifa. Tuzo inatupa nguvu mpya
za kupambana na aina zote za ukatili zikiwemo mimba za utotoni, ndoa za
utotoni kwa kuimarisha mapambano haya ambapo sasa tuna wanaharakati wa
kujitolea zaidi ya 2000 na tunafanya kazi katika mikoa zaidi ya 6 yenye
kiwango kikubwa cha ukatili”,ameongeza Ally.
Shirika
la KIVULINI (Kivulini Women’s Right Organization - Mwanza) limetangazwa
kuwa Kinara wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia , mashirika mengine ni Hope
for Girls and Women in Tanzania (Mara), Agape Organization (Shinyanga),
Tanzania’s Media Women’s Association (TAMWA) – Zanzibar, DMI Spring of
Hope (Dar es Salaam) na Shika Ndoto (Dar es Salaam).
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akiushukuru Umoja
wa Ulaya na Taasisi za Umoja wa Ulaya na Balozi mbalimbali kwa kutambua
mchango mkubwa wa shirika la KIVULINI katika kupinga ukatili wa
kijinsia na kulipa shirika lake Tuzo ya Ruzuku ambayo itakwenda kusaidia jitihada zao za kupambana dhidi ya ukatili wa kijinsia. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akielezea namna tuzo ya Kinara wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia ilivyowapa thamani
kubwa KIVULINI kwani kazi wanayoifanya inatambulika kitaifa na
kimataifa. Amesema tuzo hiyo imewapa nguvu mpya za kupambana na aina
zote za ukatili zikiwemo mimba za utotoni na ndoa za utotoni na ukatili
wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto
Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akielezea namna tuzo ya
Kinara wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia ilivyowapa nguvu ya kwenda kuwekeza
nguvu zaidi kwa wananchi na taasisi za kiserikali ili kuhakikisha
athari za ukatili wa kijinsia hazinyamaziwi na kila mmoja anakuwa sehemu
ya mabadiliko.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally (wa pili kulia) akiwa
amesimama wakati Shirika lake la KIVULINI likitangazwa kushinda Tuzo ya
Ruzuku kutokana na kuwa Kinara wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia kwenye
Tamasha la Utoaji Tuzo kwa Mashirika sita Vinara wa Kupinga Ukatili wa
Kijinsia nchini Tanzania katika Siku 16 za Uanaharakati Kupinga Ukatili
wa Kijinsia lililofanyika Serena Hotel jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally (wa pili kulia) akiwa
amesimama wakati Shirika lake la KIVULINI likitangazwa kushinda Tuzo ya
Ruzuku kutokana na kuwa Kinara wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia kwenye
Tamasha la Utoaji Tuzo kwa Mashirika sita Vinara wa Kupinga Ukatili wa
Kijinsia nchini Tanzania

Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally (wa tano kushoto)
akifuatilia matukio wakati Shirika la KIVULINI likitangazwa kushinda
Tuzo ya Ruzuku kutokana na kuwa Kinara wa Kupinga Ukatili wa
Kijinsia kwenye Tamasha la Utoaji Tuzo kwa Mashirika sita Vinara wa
Kupinga Ukatili wa Kijinsia nchini Tanzania
Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally (katikati) akifuatilia
matukio wakati Shirika la KIVULINI likitangazwa kushinda Tuzo ya Ruzuku
kutokana na kuwa Kinara wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia kwenye Tamasha la
Utoaji Tuzo kwa Mashirika sita Vinara wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia
nchini Tanzania
Wanaharakati
wa kupinga ukatili wa kijinsia wakiwa kwenye Tamasha la Utoaji Tuzo kwa
Mashirika sita Vinara wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia nchini Tanzania
ambapo shirika la KIVULINI limetangazwa kushinda tuzo ya Ruzuku kutokana
na ukinara wake katika kutokomeza mimba za utotoni, ndoa za utotoni na
ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.

Msanii
Ben Pol akitoa burudani kwenye Tamasha la Utoaji Tuzo kwa Mashirika
sita Vinara wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia nchini Tanzania ambapo
shirika la KIVULINI limetangazwa kushinda tuzo ya Ruzuku kutokana na
ukinara wake katika kutokomeza mimba za utotoni, ndoa za utotoni na
ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.
Msanii
Nandy akitoa burudani kwenye Tamasha la Utoaji Tuzo kwa Mashirika sita
Vinara wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia nchini Tanzania ambapo shirika la
KIVULINI limetangazwa kushinda tuzo ya Ruzuku kutokana na ukinara wake
katika kutokomeza mimba za utotoni, ndoa za utotoni na ukatili wa
kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.
Wasanii
mbalimbali wakitoa burudani kwenye Tamasha la Utoaji Tuzo kwa Mashirika
sita Vinara wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia nchini Tanzania ambapo
shirika la KIVULINI limetangazwa kushinda tuzo ya Ruzuku kutokana na
ukinara wake katika kutokomeza mimba za utotoni, ndoa za utotoni na
ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.
Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...