KIKOSI cha KMC FC kesho kitashuka katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kwenye mchezo wa michuano ya kombe la Azam Sports Federation ASFC dhidi ya Majimaji ya mkoani Ruvuma utakaopigwa saa 16:00 jioni.

Kikosi hicho cha Manispaa ya Kinondoni kimefanya maandalizi ya kutosha na kwamba kiko tayari kwa mchezo huo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa kama Timu inakwenda kupata ushindi na hivyo kusonga mbele kwenye michuano hiyo.

KMC FC inafanya maandalizi ya mchezo huo kwa kuzingatia kuwa michuano hiyo ipo katika hali ya mtoano na kwamba mkakati wa Timu ni kuhakikisha kuwa inaendelea kusonga mbele hadi hatua ya fainali na hivyo kuchukua kombe hilo.

Tunakwenda kwenye michuano ya ASFC ambayo kimsingi tunajua kuwa inaushindani mkubwa na ipo katika hali ya mtoano, kwamba ukifungwa ndio unakuwa umemaliza safari ya kusonga mbele, lakini pia Majimaji ni Timu nzuri na wao tunafahamu wanahitaji kufanya vizuri, hivyo tunakwenda kupambana uwanjani ili kupata ushindi.

“Hali ya kikosi iko vizuri kwa maana ya morali za wachezaji zipo juu, kila mmoja anahitaji Timu ifanye vizuri kwenye michuano hiyo kwa sababu tunamalengo makubwa ambayo ni kuchukua kombe hilo,kitu ambacho tunafahamu kinawezekana kwasababu ipo ndani ya uwezo wetu”.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...