Na Khadija Kalili, Chalinze
Hassan Rajab Mwinyikondo ameapishwa kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze Mkoani Pwani ambapo alikula kiapo hicho mbele ya Madiwani 19 wa Chama Cha Mapinduzi na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Zainab Abdallah katika halfla iliyofanyika kwenye Ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.
Akizungumzia mara baada ya kula kiapo hicho cha uongozi Mheshimiwa Mwinyikondo alisema kuwa anaahidi kuendeleza mambo yote mazuri ambayo yaliyoasisiwa na watangulizi wake.
"Chalinze ni Halmashauri nzuri na yenye utajiri mkubwa hivyo nahitaji kufanya kazi na wenzangu ikiwemo wataalamu Ili kuleta maendeleo ambayo yataandika historia kubwa kwetu na hata katika Kizazi kijacho" alisema Mwinyikondo.
"Nitahakikisha nafanya kazi kwa weledi ikiwa ni pamoja na kusimamia mapato yamakusanyo Ili kuingiza fedha serikalini na kujua kila mwezi Halmashauri imeinguza kiasi gani cha fedha ili kuweza kuendeleza miradi ya maendeleo" alisema Mwenyekiti huyo.
Mwinyikondo ambaye kabla ya kuapishwa lilifanyika zoezi la kupiga kura ambapo alipata kura 19 zilizopigwa na Madiwani 19 na hakukua na kura iliyo haribika.
Aidha Malota Kwaga amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi wa Halmashauri hiyo na yeye alipita bila kupingwa.
Hafla hiyo ya kumuapisha Mwenyekiti huyo ilishuhudiwa na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Zainab Abdallah pamoja na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bagamoyo Alhaj Abdul Sharif.
Aidha DC Zainab amewaasa Madiwani na Wabunge wote kwa pamoja kuvunja kambi zao na kuunganisha nguvu zao kwa pamoja Ili kuijenga Halmashauri ya Chalinze na kuwaletea maendeleo wananchi kwa ujumla.
adstriangle
ReplyDelete