Na.Vero Ignatus,Arusha
TUME ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) imesema kuwa ni takwa la kisheria kuhakikisha kuwa wafanyakazi wote wanaofanya kazi kwenye tasnia/sekta ya mionzi wanapata mafunzo ya Usalama
Hayo yamesemwa na Kaimu mkurugenzi mkuu wa Taec na Mkurugenzi wa Teknolojia na huduma za kiufundi Dkt Remijius Ambrose Kawala, kwamba Lengo kuu la mafunzo haya ni kuwezesha wataalamu wanaotumia vyanzo vya mionzi, waweze kujua mbinu bora ya kujikinga na madhara yanayoweza kusababishwa na mionzi, ili kulinda wafanyakazi, wananchi, wagonjwa na mazingira.
Kawala amesema Vilevile waweze kutambua viwango vya mionzi ambavyo ni salama katika maeneo ya kazi ,ili kuepuka athari zinazoweza kusababishwa na mionzi, ikiwa ni pamoja na kufuata sheria za usalama wa mionzi mahala pa kazi ,bila kusahau kuzingatia miongozo ya Kitaifa na Kimataifa inayoelekeza namna salama ya matumizi ya mionzi.
Aidha katika kaguzi 655 ambazo hufanywa na Taec kila mwaka kwa Tanzania nzima, kwa kuwaleta wadau mbalimbali, imekuwa vhachu ya watu wengi kuanza kuelewa umuhimu wa mafunzo hayo,ambapo wameanza na kuyatendea kazi za kiusalama zaidi wawapo kazini.
‘’Mafunzo haya hayawi kwasababu ya mazowea yapo kwasababu ya kuendeleza ule utamaduni mzuri wa uthibiti salama wahizi mashine za mionzi, lakini pia na kwa usalama ,kuendeleza namna njema ya viasili vinavyotumia mionzi kwaajili ya kuwalinda wafanyakazi wenyewe ,pamoja na wale wanaokwenda kutumia nikimaanisha wagonjwa wenyewe alisema Kawala’’
Shovi Sawe ni Mkuu wa kitengo cha Utafiti na Mafunzo TAEC amesema ni kawaida yao kufanya mafunzo vya mionzi ambapo kuanzia 13 dec-17 dec 2021,wanatoa kwa wanaofanya kazi mahospitalini,wanaotumia vyanzo vya mionzi ,katika uchunguzi na tiba za magonjwa kwa kutumia vyanzo mionzi
Sawe alisema kuwa mionzi isipotumika vizuri ni hatari kwa afya za watumiaji na wale ambao hawatumii,hivyo wamelenga haswa kujenga uwezo katika kinga ya mionzi, ili waweze kupata faida wanayoitegemea katika kazi zao, wagonjwa ,wananchi,pamoja na wao wenyewe walinde dhidi ya madhara mabaya yanayoweza kutokea kutokana namstumizi yadiyo sahihi ya q mionzi
Amesema kuwa mionzi imegundulika kuwa na faida ambazo chunguzi za aina nyingine haziwezi kufanya,huku akitolea mfano wa upigaji picha mguu uliovunjika, kuwa mionzi imethibitisha ufanisi mkubwa kuliko aina nyingine, hivyo ifahamike kuwa hakuna kitu chenye faida tu bila kuwa na madhara hivyo basi, umefikia wakati wa kujifunza namna ya kutumia mionzi kupata kile wanachotegemea na kubakia salama
Daniel Mariki ni Mteknolojia mionzi katika hospitali ya KCMC Moshi Kilimanjaro ambaye ni mmoja wa washiriki mshiriki wa darasa hilo la siku tano ,amesema kuwa mafunzo hayo yanatija kubwa kwao, kwani watapata maelekezo mbalimbali ya namna ya kutumia vifaa hivyo vya mionzi kwa usahihi zaidi
Mariki anasema yeye kama mtumiaji wa vifaa hivyo,itamsaidia kufahamu kuwa kina ubora kiasi gani na kinatoa dozi sahihi kwa magonjwa ,hivyo mafunzo hayo yatawaimarisha wao kama wateknolojia kwa suala zima la kumuhudumia mgojwa na jamii kwa ujumla
Hellen Deogratius kutoka hospital ya Uhuru Dodoama amesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kujilinda wao pamoja na wagonjwa wanao wahudumia wawapo kazini,hivyo wameishukuru Tume kwa kuhakikisha wao wanakuwa salama
‘’Mafunzo haya yanatusaidia kuhakikisha kuwa tunatoa dozi sahihi kwa watu tunaowahudumia vilevile sisi wenyewe tunakuwa salama bila kudurika na tutawalinda wengine.Alisema Hellen
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...